HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 17, 2023

BENKI YA STANDARD CHARTERED YAELEZA DHAMIRA KUENDELEZA JAMII KIUCHUMI.

BENKI ya Standard Chartered  Tanzania imesisitiza dhamira yake ya kuendeleza  mbele gurudumu la maendeleo ya wananchi  kiuchumi nchini.

Hivi karibuni Benki hiyo,ilifikia makubaliano na Benki ya Access Plc kuhusiana na huduma za kibenki kwa  wateja,  binafsi na biashara.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na  Benki hiyo  leo Jijini Dar es Salaam imesema kuwa Benki ya Access itasimamia huduma za kibenki  kwenye nchi zilizotajwa hapo juu.

Taarifa hiyo ilisema kuwa huduma zilizotajwa hapo juu zitabaki zitategemea kutoka kwa mdhibiti wa Benki hiyo nchini Nigeria.

Access Bank ina  mtandao wa zaidi ya matawi 600 katika mabara matatu,masoko 18 na wateja wanaofikia milioni 52.

Benki ya Standard Chartered   na Access Bank Plc (Access) zilifikia makubaliano ya kuuza hisa za Standard Chartered katika kampuni zake tanzu za  nchini  Angola, Cameroon,Gambia na   Sierra Leone, pamoja na Biashara yake ya wateja,Binafsi na Biashara ya Benki nchini Tanzania ,kwa kutegemea idhini ya udhibiti.

Benki ya Access itasimamia shughuli zote katika nchi zilizotajwa, na kuhakikisha uendelevu kwa wafanyakazi na wateja. Mpito huo unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 12 ijayo.

Taatifa hiyo imebainisha wazi kuwa  nchini Tanzania, haitajiondoa kutoa huduma za Biashara kwa wateja,Binafsi na biashara ya Benki maarufu kama rejareja ili ku shughukika za kibenki kwa  mashirika na Taasisi.

Access Benki itatoa huduma mbalimbali za kibenki na uendelevu wanhuduma  kwa wateja wake ikiwemo  waajiriwa na wateja wa iliyokuwa Standard Chartered Benki katika nchi tano zikizotajwa hapo juu.

Benki ya Access Bank na  Standard Chartered ziitafanya kazi kwa karibu katika kipindi cha mpito cha miezi 12 ijayo. work closely together in the
 
Akizungumzia makubaliano yalifikiwa Mtendaji mkuu wa Benki  ya Standard Charter Tanzania, Herman Kasekende,alisema kuwa  Benki hiyo imekuwepo chini kwa zaidi ya miaka 106 na ina  amini katika mipango ya nchi ya muda mfupi na mrefu..

 Kasekende aliwahakikishia wateja wa benki hiyo kuwa huduma zote na mtandao wa benki zitaendelea kutolewa kwa makubaliano na Acceas Benki.

  "Tunaamini tumefikia mafanikio makubwa  zaidi kwa kuwafanya wateja wetu watuamini kama ni sehemu pekee ya wao kuwekeza," alisema mtendaji mkuu huyo.

“Wakati mipango ijayo ya benki ,tumefarijika na ukuaji na ustawi wa benki yetu katika Bara la Afrika na dhamira ya Benki inabaki ileile ya kuwahudumia watanzania," aliongeza.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad