TAASISI ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kujulisha Umma kwamba kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya kuzibua mishipa ya damu ya miguu (Peripheral Interventions) iliyopaswa kufanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Andulusia ya nchini Misri iliyopangwa kufanyika tarehe 19-21/06/2023 imeahirishwa hadi tarehe 15-19/07/2023.
Wagonjwa wote waliofanyiwa uchunguzi na kuandaliwa kwaajili ya kupata matibabu katika kambi hiyo watapigiwa simu na kupewa taarifa zaidi.
Tunaomba radhi kwa ndugu, jamaa na wagonjwa kutokana na usumbufu uliojitokeza.
Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0754870969 Dkt.George Longopa, 0745836938 Dkt. Dickson Minja na 0788308999 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.
“Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”.
Imetolewa
Anna Nkinda
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment