Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), imefanya uzinduzi wa mfumo wa maombi ya vibali na usajili wa ndege zisizokuwa na rubani maarufu kama “drones” uliofanyika Makao Makuu ya TCAA,Ukonga Banana jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCAA ambaye pia Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi TCAA,Bw. Daniel Malanga amesema Mamlaka ilichapisha taarifa juu ya kuanza kutumika kwa kanuni za matumizi ya ndege zisizokuwa na rubani ya
Mwaka 2018, ‘The Civil Aviation (Remotely Piloted Aircraft System) Regulations 2018’, ambazo zinamtaka mtumiaji wa ndege hizo kuwa na vibali na kuzisajili.
Amesema changamoto mbalimbali zimekuwa zikijitokeza kwenye eneo la utoaji wa vibali na usajili wa ndege zisizokuwa na rubani tangu kuanza kwa utekelezaji wa kanuni hizo mnamo mwaka 2020, hivyo mfumo huu mpya umelenga kupunguza changamoto hizo.
"Mfumo huu sasa muombaji ataweza kuwasilisha maombi mbalimbali ikiwemo, vibali vya kuingiza ndege zisizokuwa na rubani. (Drone import permit), vibali vya kutoa ndege zisizokuwa na rubani (Drone export permit), vibali vya kutumia ndege zisizokuwa na rubani akiwa hapa nchini (drone operations permit), na usajili wa ndege zisizokuwa na rubani (Drone registration). Alisema Malanga
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Daniel Malanga akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA).Hamza Johari kuhusu uzinduzi wa mfumo wa maombi ya vibali na usajili wa ndege zisizokua na rubani maarufu kama “drones” uliofanyika Makao Makuu ya TCAA,Ukonga Banana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti Uchumi Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Daniel Malanga akizundua mfumo wa maombi ya vibali na usajili wa ndege zisizokua na rubani maarufu kama “drones” kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA).Hamza Johari.
Meneja TEHAMA TCAA Goodluck Msangi akielezea mfumo wa maombi ya vibali na usajili wa ndege zisizokua na rubani maarufu kama “drones” wakati wa uzinduzi wa mfumo huo uliofanyika Makao Makuu ya TCAA,Ukonga Banana jijini Dar Es Salaam.
Mkaguzi wa Ndege zisizokuwa na Rubani TCAA Ibrahim Abdallah akitolea ufafanuzi swali lililoulizwa na mwandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mfumo wa maombi ya vibali na usajili wa ndege zisizokua na rubani maarufu kama “drones” uliofanyika Makao Makuu ya TCAA,Ukonga Banana jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka wakifuatilia uzinduzi wa mfumo wa maombi ya vibali na usajili wa ndege zisizokua na rubani maarufu kama “drones” uliofanyika Makao Makuu ya TCAA,Ukonga Banana jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment