HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 19, 2023

RAIS WA ZANZIBAR MGENI RASMI SIKU YA MAAFISA UTUMISHI NA MAAFISA UTAWALA TANZANIA MEI 20, 2023

 

Mwenyekiti wa  Maafisa Utumishi na Maafisa Utawala Tanzania (THRAPA) Gerald Ruzika akizungumza na Maafisa Utumishi na Maafisa Utawala ikiwa ni kuelekea maadhimisho siku ya siku yao ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Mei 20, kila mwaka.Mkutano huo unafanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanzia Mei 18-20, 2023.

KUELEKEA siku ya Maafisa Utumishi na Maafisa Utawala duniani ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Mei 20, Chama cha kitaaluma cha Maafisa Utumishi na Maafisa Utawala Tanzania (THRAPA) kinafanya Mkutano mkuu wa mwaka kuanzia Mei 18 hadi 20 ambapo itakuwa kilele chake, Mkutano huo umefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam(J)

Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Husein Mwinyi anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mei 18,2023 Mwenyekiti wa THRAPA, Gerald Ruzika amesema kuwa mkutano huo umejumuisha wataalamu wa kada zote mbili ambazo zilikuwa hazitambuliki sasa taaluma hizi zitakuwa zikitambulika kwani watakuwa wanakutana kila mwaka ili jamii ijue kuwa taaluma hiyo ipo.

"Kada hii kwa kiasi flani imekuwa haitambuliki, sasa tunataka nchi hii ijue."

Tunatangaza kada hii ipo na sio kila mtu anaweza akafanya kazi ya Rasilimali watu au akafanya kazi ya utawala, zipo changamoto katika kada hii, kubwa zaidi ni hii ya la kutokutambulika, lakini wakati mwingine watu kudhani kwamba kazi hii inaweza ikafanywa na mtu yeyote sio kila mtu anaweza kuteuliwa akafanya kazi hizi". Amesema Ruzika

Amesema kuwa wanataka watanzania kujua kada hizi zipo zinatambulika na inathaminiwa na taasisis yeyote rasilimali watu ndio moyo wa taasisi.

"Kwenye taasisi lazima atambulike mtu anayesimamia rasilimali watu na taaluma inayotambulika duniani ni rasilimalinwatu".

Amesema kuwa kama taasisi itakuwa haina rasilimali watu inayofanya kazi katika taasisis basi lazima mambo yaende kombo.

Kwa upande wa Mweka hazina Mkuu wa THRAPA, Christopher Mwasansu amewakaribisha wanachama wa chama hicho kufika katika mkutano huo mhimu kwa mstakabali wa taaluma yao, amesema kunamambo mhimu ya kujadili.

Amesema kuwa watabadilishana uzoefu na kujengeana uwezo wa kuweza kuongoza katika taasisi na kampuni mbalimbali.

Akizungumzia taaluma hiyo ameifananisha na mchezaji wa Mpira timu Simba, Clatous Chota Chama jinsi anavyopiga mwingi na ndivyo wanakada hiyo walivyo mhimu katika taasisi na kampuni mbalimbali.

"Ni watu mhimu kwenye taasisi kwenye kampuni na ni kiungo kati ya waajiri na waajiriwa." Amesema Mwansasu

Amesema sasa wanakwenda kuweka mapinduzi ya taaluma ili taaluma hiyo iweze kutambulika na kuwa na nguvu ya kusimamia rasilimali watu na utawala nchini.

Akizungumzia umoja huo mtunza hazina mkuu, Grofrey Projest amesema umoja huo utakwenda kusimama na kuwa imara na kuwa na nguvu nchini kwa sababu umoja huo unajengwa na watu wanaoshikiria sehemu mhimu za kiutawala wa kampun na taasisi mbalimbali.




Baadhi ya Maafisa Utumishi na Maafisa Utawala Tanzania (THRAPA) wakisikiliza mada ikiwa ni kuelekea maadhimisho siku ya siku yao ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Mei 20, kila mwaka.Mkutano huo unafanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanzia Mei 18-20, 2023.








Matukio mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad