HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 19, 2023

HUDUMA ZA KIBINGWA ZA MOYO HOSPITAL YA KISARAWE KUPUNGUZA IDADI YA RUFAA

 




Na Mwamvua Mwinyi, Kisarawe
KIONGOZI wa mbio za Mwenge Kitaifa Abdallah Shaib,amezindua huduma za kibingwa za moyo katika hospital ya wilaya Kisarawe Mkoani Pwani.

Akizungumza baada ya kuzindua mradi huo wakati Mwenge wa Uhuru ulipopita kujionea wilaya ilivyosimamia na kutumia kwa ufanisi mapato ya ndani katika kuboresha huduma za afya ,Shaib alieleza Serikali inaendelea kuboresha kwa kasi Mazingira ya huduma za afya na kuongeza miundombinu.

Alisema, kwa hakika huduma hizo zinakwenda kuwaondolea wananchi kero ya kufuata huduma za kibingwa za moyo katika hospital nyingine kubwa zinazotoa huduma hizo.

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe,dkt.Alhaj Seleman Jafo alibainisha kwamba, hospital ya wilaya ya Kisarawe ni ya kwanza nchini kutoa huduma za kibingwa za magonjwa ya moyo.

"Ninaishukuru Serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya maboresho ya huduma za afya nchini na kuiwezesha hospital hii kuwa ya kwanza nchini kutoa huduma hizo"alifafanua Jafo.

Mganga mkuu wa wilaya ya Kisarawe Zaituni Hamza akitoa taarifa ya mradi alieleza, Huduma hizo zitapunguza umbali mrefu wa km.150 kufuata huduma za kibingwa za moyo Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete Mkoani Dar es Salaam .


Pia zitapunguza idadi ya rufaa kwa wagonjwa kutoka wagonjwa watano hadi mgonjwa mmoja kwa mwezi
na kuongeza utambuzi wa mapema wa magonjwa ya moyo, kuwapunguzia wananchi muda na gharama za nauli hivyo kuwapa nafasi ya kufanya shughuli za kujiongezea kipato ili kuinua uchumi wao na Taifa kwa ujumla.


Zaituni alieleza,lengo la mradi ni kusogeza huduma za kibingwa za magonjwa ya moyo karibu na wananchi katika kipindi cha mwaka 2021/2022.


Anasema, Jumla ya wagonjwa 179,702 waliopokea huduma kati ya wagonjwa 3,246 waligundulika kuwa na ugonjwa wa shinikizo la juu la damu,ambalo ni moja kati ya visababishi vya magonjwa ya moyo.


Akipokea mbio za Mwenge wa uhuru ukitokea wilaya ya Kibaha Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Fatuma Nyangasa alieleza, mwenge huo utakimbizwa umbali wa kilometa 146.5 katika Tarafa tatu za Sungwi,Chole na Maneromango kata Tisa kati ya 17 na umepita kwenye vijiji 21 kati ya 65 .


Nyangasa alisema,Mwenge huo umepitia miradi 11 yenye thamani ya Bilioni 2.451.4 ambapo kati ya fedha hizo Serikali kuu sh.1,154,627,124 , Halmashauri ya wilaya sh.38,830,000 na wahisani sh.403,383,753 mchango wa Mwenge sh.5,000,000 nguvu za wananchi 200,000 na wawekezaji 851,840,361 .


Nyangasa alisema,michango ya Mwenge imetumika pia kununua vitanda vya wanafunzi shule ya Sekondari Jokate Mwegelo na mashine ya kuchujia maji kwa kikundi cha vijana UVIKI .

Mwenge huo umetembelea Mradi wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, hifadhi ya Mazingira na Utunzaji wa vyanzo vya maji na uhifadhi unavyochangia pato la Taifa (USHOROBA) Msitu wa Pugu Kazimzumbwi na kiwanda cha usindikaji maziwa CHAWAKIMU.

Mradi mwingine ni pamoja na mradi wa jengo la baba,mama na mtoto kituo cha afya Masaki na kutembelea eneo maalum la upandaji miti 500 msitu wa Kazimzumbwi na mradi wa bweni la wasichana shule ya Sekondari ya wasichana Jokate Mwegelo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad