HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 18, 2023

MWENGE WA UHURU WAMULIKA KIWANDA CHA TANBREED POULTRY LIMITED, WAAGIZWA WAWEKE MAZINGIRA SALAMA KWA WAFANYAKAZI

 


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kibaha Mji Mhandisi Mshamu Ali  Munde  akiupokea mwenge leo asubuhi katika viwanja vya Visiga Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Halmaahauri ya Mji Kibaha Mussa Ndomba akifuatiwa na aliyekua Mkuu wa Mkoa Mstaafu Mhandisi  Evarist Ndikilo na  aliyekua Mkuu wa Wilaya wa tatu nchi nzima  na DC wa Kwanza wa Wilaya ya Kibaha  mwanamke Bi Mary Luwilo.


Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim akikagua bidhaa za wajasiriamali ambao walikua waraibu wa dawa za kulevya.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon  akifafanua jambo leo kwenye Mbio za Mwenge Uhuru uliopokelewa katika Viwanja vya Visiga  Kibaha Makoani Pwani.


Na Khadija Kalili
KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim amewataka viongozi wa Kiwanda cha Tanbreed Poultry Limited kuwajali wafanyakazi wake kwa kuwawekea mazingira mazuri ya kazi na kuwapa vifaa vya kuwakinga wasiweze kupata madhara wawapo kazini.

"Kiongozi huyo amesema hayo leo alipotembelea kiwandani hapo huku akiwangoza viongozi akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na wananchi katika mbio za mwenge Wilayani hapa.

Amesema hayo baada ya kutembelea Kiwanda hicho kinachomilikiwa na kufanya biashara sambamba na Kampuni dada ya Interchick Company Limited na Tanzania Breeder and feed mill ambapo kiwanda hiki ni tawi la Kiwanda kilichopo Dar es Salaam ambapo pia kiwanda hiki kimeanza kufanya kazi Aprili 2022.

Meneja waKiwanda hicho cha Tanbreed Poultry Limited Dickson Gerald Malamsha ameahidi kufanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Taifa Abdullah Shaib Kaim.

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon amesema kuwa kaulimbiu ya mwenge wa Uhuru 2023 inasema 'Tunza Mazingira Okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa Viumbe hai kwa uchumi wa Taifa'.

Amesema hayo leo ikiwa ni kwenye mwendelezo wa mbio za Mwenge Wilayani Kibaha Mkoani Pwani uliotembelea miradi mbalimbali Wilayani Kibaha.

Mwenge huo umepokelewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Ali Munde aliyepokea mwenge huo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kibaha Vijijini Butamo Ndalahwa

"Sisi wananchi wa "Halmashauri ya Kibaha Mji tunafuraha kubwa kuupokea Mwenge wa Uhuru"amesema Nickson. "Halmashauri ya Kibaha ina eneo la ukubwa wa Km.750 sawa na ekari185,276.Kiutawala ina Tarafa 2,Kata14 na mitaa73,kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa sasa lwa pamoja tuungane katika

kukabiliana na changamoto za dawa za kulevya kwa vijana wetu iliwemo kuwapa malezi bora na kuzingatia imani za dini mila na desturi zetu .

Wakati huohuo Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Shaib amekagua mradi wa barabara ya Viwatilifu kwenye kipande cha urefu wa Mita 400 kwa kiwango cha lami barabara hiyo inaanzia kwenye makutano ya barabara ya TAMCO hadi Mnarani (1.03 Km) na inapita katika eneo la uwekezaji wa viwanda manufaa ya mradi huu ni kuimarisha maendeleo ya jamii na ukuaji wa uchumi" amesema Meneja wa TARURA Wilaya ya Kibaha Samuel Ndoveni.

Ndoveni amesema kuwa mradi huu umetekelezwa na Mkandarasi M/S Mirogenia Investment CO.Limited ya Jijini Dar es Salaam wenye thamani ya Mil.496,755,000 kwa muda wa miezi sita ,mradi huu ulianza Septemba 2021 na ulitegemewa kukamilika Machi mwaka huu lakini kutokana na mvua na kuchelewa kwa msamaha wa kodi (VAT exemption)kumesababisha kuongezeka muda wa kumaliza mradi mpaka ifikapo Agosti mwaka huu.

Amesema kuwa wamepata ushirikiano mkubwa wakati wa utekelezaji wa mradi na wamepata ushirikiano mzuri kutoka kwa viongozi wa Mkoa wa Pwani,Wilaya, Halmashauri na Kata katika kutatua changamoto mbalimbali zilizojitokeza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad