HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 25, 2023

MKUTANO MKUU WA KUMI WA TAPSEA WAFUNGULIWA RASMI LEO, ZANZIBAR

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais - Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Haroun Ali Suleiman akizungumza wakati akifungua rasmi ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa kumi wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania, unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Zanziar (SUZA), mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. Mkutano huo ulianza jana kwa kutanguliwa na Semina ya kitaaluma iliyotolewa na Taasisi mbalimbali ikiwa ni kuendelea kuwajega kitaaluma Makatibu Muhtasi wote nchini.

======   ======  ======

Na Tatyana Celestine, Zanzibar 

Mei 25, 2023: Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Rais wa awamu ya sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeanza utekelezaji wa kushughilikia changamoto za Makatibu Mahsusi Tanzania ikiwemo kuandaa Mtaala na stahiki zao kwa lengo la kutengeneza wanataaluma kuwa msaada katika kuwalinda mahala pa kazi

Akizungumza kwa Niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene,  Naibu Waziri Ridhiwani Kikwete amewahahakishia Makatibu Mahsusi Tanzania kuwa tayari Serikali imeshaanza kutoa maelekezo kuwa Mitaala hiyo ifanane na Taaluma yao ili kuwafanya wawe na sifa kimataifa.

Aidha amesema kuwa Suala la Maslahi ya Makatibu Mahsusi Tanzania tayari Serikali imeanza kushughilikia kwa kuwapandisha vyeo, ubadilishwaji Kada na kuwaingiza kwenye mfumo stahiki itakayopelekea kuondoa malalamiko baina yao kwa kutengeneza matabaka.

Vilevile Naibu Waziri Kikwete amesema kuwa Serikali imedhamilia kuwapa thamani yao kikamilifu Makatibu Mahsusi hao na ndio maana Rais ameitisha agizo la wao kukutana Zanzibar kutunukiwa vyeti baada ya mafunzo lakini pia kupata kiapo kwa pamoja kitakachowaongoza katika utendaji wa kazi zao.

Naye Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Haroun Suleiman amewaahidi Makatibu Mahsusi Tanzania kushughulikia kikamilifu kama ombi lililotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Zuhura Maganga hapo awali aliposoma risala na kusema kuwa ni agizo la Rais Samia na pia itaandikwa historia kwa tukio la kiapo litakalowakutanisha Rais, Mawaziri na viongozi wengine wa Serikali katika kilele cha mkutano huo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete akizungumza wakati akitoa salamu katika ufunguzi rasmi ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa kumi wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania, unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Zanziar (SUZA), mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. 
Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Zuhura Maganga akizungumza katika ufunguzi rasmi wa Mkutano Mkuu wa kumi wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania, unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Zanziar (SUZA), mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Rashid Hadid Rashid akichagiza wanachamawa wa TAPSEA katika ufunguzi rasmi wa Mkutano Mkuu wa kumi wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania, unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Zanziar (SUZA), mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. 
Katibu wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA), Anneth Charles Mapima akizungumza katika ufunguzi rasmi wa Mkutano Mkuu wa kumi wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania, unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Zanziar (SUZA), mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. 
 
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad