HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 25, 2023

BANDARI TANGA WAZUNGUMZIA FAIDA LUKUKI MABORESHO YALIYOFANYIKA,KUWA NA UWEZO WA KUPAKUA TANI MILIONI TATU KWA MWAKA

 
-Uongozi wasema bandari hiyo imezaliwa upya, watanzania waitumie

Na Mwandishi Wetu,Tanga

UONGOZI wa Bandari ya Tanga umeelezea hatua kwa hatua maboresho makubwa ambayo yamefanywa katika bandari hiyo, hivyo umewaomba Watanzania kuitumia bandari hiyo katika kusafirisha na kupokea mizigo yao.

Aidha umesema kwamba bandari ya Tanga kwa sasa imekuwa na uwezo mkubwa wa kupokea meli kubwa huku ukifafanua kwa mwaka watakuwa na uwezo wa kupakua tani milioni tatu kutoka tani 750,000 kwa mwaka.

Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea bandari hiyo, Meneja Bandari ya Tanga Masoud Mrisha amesema baada ya maboresho makubwa kufanyika bandari hiyo imezaliwa upya na Watanzania kutoka mikoa ya kaskasini na mikoa jirani waitumie.

“Watanzania waje waitumie bandari yetu mizigo inashuka kwa usalama na hakuna wizi wowote, huduma inapatikana kwa ubora wa juu na tunafanya kazi kwa saa 24 kwa siku zote saba za wiki.

Amefafanua kutokana na ushirikiano mkubwa ambao wanaupata kutoka kwa viongozi wa Chama na Serikali ndio umefanikisha kuifanya bandari hiyo kuwa ya kisasa kutokana na maboresho yaliyofanywa na Serikali kwa kutumia mabilioni ya fedha.

Akielezea zaidi historia ya bandari hiyo amesema ilianza kujengwa mwaka 1888 na kukamilika mwaka 1891 ilikuwa inajulikana kwa jina la Marine Jet huku gati la kwanza la kwanza lilianza kujengwa mwaka 1914 na gati la 1954 , magati yote mawili yalikuwa na urefu wa mita 450

“Bandari ya Tanga ina kubwa wa eneo hekta 17 , pia kuna maeneo mengine ya Mwambani kilometa sita kutoka hapa lina ukubwa wa hekta 176 , Chongoleean ambako linajengwa bomba la mafuta ambalo liko kilometa 28 na lina ukubwa wa hekta 207

“Pia tuna bandari ndogo ikiwemo ya Pangani ,Kipumbwi, Kaja na Sahare.Tunao wafanyakazi 258 kati ya hao wanaume 199, na wanawake 59 , bidhaa kubwa ambazo tunasafirisha kwenda nje ya nchi kupitia bandari hii ni katani, kahawa, mbao na karanga pori.”

Amefafanua katika kipindi chote hicho tangu kuanza kwa bandari hiyo meli zote kubwa zilikuwa zinasimama umbali wa kilometa 1.7 na mzigo ule unapopakuliwa huamishwa kwenye matishari, na kukokotwa hadi getini, hivyo kutokana na hali hiyo Serikali iliamua kufanya maboresho.

“Serikali kupitia TPA iliona hilo na kufikia mwaka 2019 kulianza mradi wa kuboresha bandari ya Tanga uliokuwa na awamu mbili, awamu ya kwanza ilianza Agosti 3,2019 na kazi kubwa iliyofanyika ni kuongeza kina cha maji kwenye mlango bahari, kutoka kilometa 1.7 mpaka kilometa 13.

“Na upana mita 73, kuongeza kina cha maji sehemu ya kugeuzia meli kutoka mita 3 mpaka 13 kwa kipenyo cha mita 800.Pia awamu ya kwanza ilijumuisha ununuzi wa vifaa kwa ajili ya shughuli za bandarini hapo.Mradi wote huo wa kuongeza mlango bahari, sehemu ya kugeuzia meli pamoja na ununuzi wa vifaa awamu kwanza uligharimu Sh.bilioni 172 .3,”amesema Mrisha.

Kuhusu awamu ya pili ya mradi amesema ulihusisha maboresho ya kuboresha gati mbili , gati ya kwanza iliyojengwa mwaka 1914 na ile gati ya mwaka 1954 ambapo kilichofanyika upande wa Mashariki waliingia majini kwa mita 50 na Magharibi waliingia mita 92 na kuongeza kina cha maji kutoka mita 3 mpaka 13 .

Amesema mradi huo wa awamu ya pili ulianza Septemba 5 mwaka 2020 na ulikuwa wa miezi 22 , thamani yake ni Sh.bilioni 256.8 na kwamba mpaka sasa umekamilika kwa 99.85 na hizo asililimia 0.15 ni vitu vidogo tu ambavyo vinasubiriwa kukamilika.

“Uwezo wa bandari kuhudumia meli kubwa mpaka hapa tunapozungumza baada ya huu mradi kukamilika tumeshaingiza meli sita zenye urefu wa mita 150 mpaka 200 kwa kipindi hiki cha miezi mitatu , shehena itaongezeka kutokana na kuhudumia meli kubwa.

“Kabla ya mradi tulikuwa na uwezo wa kuhudumia tani 750,000 lakini baada ya maboresho haya sasa tutakwenda mpaka tani milioni tatu kwa mwaka. Kama nilivyoeleza kabla ya maboresho tulikuwa na gharama kubwa za uendeshaji kutokana na kufanya kazi mara mbili ya kupakua na kupakia, gharama za mafuta zimepungua.

“Hivyo gharama za uendeshaji zimepungua na faida ya tatu meli ambayo ilikuwa inahudumiwa kwa siku nane sasa inaweza kuhudumiwa kwa siku nne,”amesema wakati anafafanua kuhusu faida za kukamilika kwa maboresho ya bandari hiyo.

Kwa upande wake Mwakilishi wa kampuni ya TodMax inayojihusisha na shughuli za 'Clearing & Forwading' Thorea Khalfan amesema kuwa anampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha uboreshaji mkubwa wa bandari mkoani Tanga unafanyika.


Kwa upande wake, mmoja wa wadau wa Bandari ya Tanga, Thorea Khalfan ambaye ni afisa mauzo kutoka kampuni ya kutoa huduma ya kutoa mizigo bandarini ya TopMax (T) Limited amesema, baada ya maboresho makubwa yaliyofanyika katika bandari ya Tanga ufanisi umeongezeka ambapo gharama za mipakuo (double handling) zimeondoshwa huku ikiwa hakuna msongamano wowote.

Thorea ameipongeza serikali ya awamu sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuatia maboresho yaliyofanyika katika bandari hiyo na kuongeza kuwa hatua hiyo itatachochea ukuaji mkubwa wa uchumi katika Taifa.

Bandari ya Tanga ni moja ya bandari kongwe nchini ambayo ujenzi wake ulianza mwaka 1988 na kukamilika mwaka 1991 ikiwa na ukubwa wa hekta 17 ikiwa na bandari ndogo ndogo nne ambazo ni Sahare, Pangani, Kipumbwi na Mkwaja ambapo miongoni mwa bidhaa zinazosafirishwa na bandari hii ni pamoja na Katani, Kahawa, mbao na macadamia (karanga


 Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha akizungumza na baadhi ya Waandishi wa habari waliotembelea bandari hiyo leo mkoani huo na kuelezwa maboresho makubwa yaliyofanyika katika bandari hiyo
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakizungumza na Meneja Bandari ya Tanga Masoud Mrisha kuhusu maboresho mbalimbali yaliyofanyika katika bandari hiyo


Baadhi ya mitambo ya kisasa iliyopo ndani ya bandari hiyo

 
 Mmoja wa wadau wa Bandari ya Tanga, Thorea Khalfan ambaye ni afisa mauzo kutoka kampuni ya kutoa huduma ya kutoa mizigo bandarini ya TopMax (T) Limited akieleza namna watakavyonufaika na maboresho makubwa ya bandari hiyo ya Tanga.




Muonekano wa maboresho ya bandari ya Tanga yaonekanavyo pichani

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad