Mkurugenzi wa Forodha na Ushuru
wa bidhaa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo anayesimamia majimbo
ya Haut Katanga, Lualaba, Tanganyika na Lomami Bw. René Kalala Masimango
na ujumbe wake umeipongeza Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa
Bandari Tanzania TPA na Wafanyakazi wake, kwa utendaji mzuri na kutoa
huduma zenye ufanisi katika Bandari zake.
Pongezi hizo wamezitoa
tarehe 04 Mei,2023, walipotembelea Makao Makuu ya TPA na Bandari ya Dar
es Salaam ili kujionea shughuli mbalimbali za kiutendaji Bandarini hapo.
“Bandari
hii ya Dar es Salaam ni muhimu sana kwa mizigo inayokuja Kongo na
inahudumia mizigo mingi , tumekuja kuona utendaji kazi wake na tumeona
kuwa kazi ni nzuri na Bandari inamipangilio mizuri.” alisema Bw.
Masimango.
Akiwakaribisha Wageni hao, Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw.
Plasduce Mkeli Mbossa, amewashukuru kwa ziara yao na amewahakikishia
kuwa Menejimenti yake ipo tayari kutatua changamoto zozote zikijitokeza
katika kuhudumia Shehena ya mzigo unaoenda na kutoka Kongo kupitia
Bandari za Tanzania kwa lengo la kulinda mahusiano mazuri na ya muda
mrefu ya kidiplomasia na Biashara Kati ya nchi hizi mbili.
“
Menejimenti ya TPA itaendelea kuzifanyia kazi changamoto zozote Katika
kuhudumia Shehena ya Kongo na kuboresha mahusiano ili shughuli
zinazofanywa na TPA Katika Bandari zake ziwe na manufaa kwa DRC.”
alisema Bw. Mbossa.
Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini DRC
Mhe. Said Juma Mshana amesema ziara hiyo ni fursa ya kuwa na
majadiliano ya pamoja na yenye tija kuhusu changamoto zinazoyakabili
mahusiano ya kibiashara na kutafuta suluhisho kwa manufaa ya Tanzania na
DRC.
“ Ziara hii itasaidia kukuza mahusiano ya kiuchumi na ya
kijamii pamoja na kuimarisha uchumi wa nchi hizi mbili pamoja na uchumi
wa Jumuiya za Kikanda.” alisema Balozi Mshana.
Naye Balozi wa DRC
nchini Tanzania Mhe. Jean Pierre Massala amesema ni ziara hii ni muhimu
sana kwa mahusiano Kati ya DRC na Tanzania na muhimu ni kufanya kazi
kwa pamoja kwa faida ya nchi hizi mbili.
“ Ni vema kuwa na mawazo
chanya katika kuimarisha Biashara kati ya DRC na Tanzania kwa faida za
kiuchumi kwa nchi hizi na Watu wake.” alisema Balozi Massala.
Taifa la Kongo ni kinara kwa kupitisha kiwango kikubwa cha Shehena Katika Bandari za Tanzania hasa Bandari ya Dar es Salaam.
Thursday, May 4, 2023
MKURUGENZI WA FORODHA NA USHURU DR CONGO ATEMBELEA TPA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment