HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 23, 2023

DKT.MWINYI AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI WA QATAR KUJA TANZANIA

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi baada ya kuwasili jana usiku jijini Doha, Qatar akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano mkubwa wa Jukwaa la Kimataifa la tatu la Uchumi utakaofunguliwa kesho.


Katika ziara yake Rais Dk. Mwinyi leo asubuhi amekutana na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Qatar Mhe. Muhamed Bin Ahmed Al-Kuwari na wadau kutoka sekta binafsi ya Viwanda.

Dk. Mwinyi aliwakaribisha wafanyabiashara hao wakubwa kuwekeza Zanzibar kutokana na fursa zilizopo pia aligusia eneo jipya la uwekezaji ambalo ni utalii wa kumbi za mikutano.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa ZIPA Shariff Ali Shariff alieleza umuhimu wa kukutana kwa Mabaraza ya uwekezaji ya Zanzibar na Qatar ili kuimarisha uhusiano zaidi.

Pia alielezea fursa za uwekezaji zilizopo Zanzibar zaidi kwa upande wa utalii kwani ujenzi wa hoteli kubwa za kifahari unahitajika kutokana na soko la utalii kuongezeka.

Kwa upande wa Tanzania bara, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Gilead J. Teri aliainisha vivuvito vilivyowekwa na serikali kusaidia kulinda mitaji ya wawekezaji kwa kipindi cha uwekezaji, na kuongeza kuwa zipo fursa kwenye sekta za Utalii, Madini, Ujenzi ikiwemo mji mkuu Dodoma, Viwanda, na huduma za kifedha na bima.

Kwa upande za Zanzibar, fursa nyingine alizowakaribisha kuwekeza ni ukodishaji wa visiwa vidogo.

Halikadhalika aliwafahamisha kwa undani fursa zilizopo katika sera ya uchumi wa Buluu ambayo imewagusa zaidi wawekezaji hao hasa suala la uchimbaji wa gesi na mafuta.

Eneo jingine ni shamba la Makurunge Bagamoyo ambalo ni mali ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar linalofaa kwa utalii na hata kilimo.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad