HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 12, 2023

AFUNGWA MIAKA 30 JELA KWA KUBAKA MWANAFUNZI KIBAHA

 Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

MAHAKAMA ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani imemhukumu Mangode Rajabu (23), Mkazi wa Soga, Kibaha kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi (jina linahifadhiwa).

Hukumu hiyo ya kesi ya jinai namba 4/ 2023 imetolewa na Hakimu Fahamu Kibona wa mahakama ya Wilaya ya Kibaha wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa hukumu.

Baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote, Fahamu Kibona alieleza amejiridhisha kumtia hatiani mshitakiwa huyo kwa Mujibu wa kifungu 130 (1), (2) (a) na kifungu 131 (1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Ilielezwa kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Novemba 7,2021 huko Soga,Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad