HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 14, 2023

Tunawajibu kulinda mazingira katika sekta ya usafiri majini :Mkeyenge:

Meneja wa Mradi wa Nairobi Convention wa Shirika la Umoja wa Mataifa linashughulikia Mazingira  (UNEP)  Dkt. Jared Bosire akitoa maelezo kuhusiana miongozo ya kufuata wakati wa ujenzi wa bandari au upanuzi katika kuepukana na madhara ya kimazingira , jijini Dar es Salaam. 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Kaimu Abdi Mkeyenge  akizungumza wakati wa akifungua warsha ya kukuza uelewa wa masuala ya mazingira kwa Nchi zilizo katika Ukanda wa Magharibi wa Bahari ya Hindi , Jijini Dar es Salaam.
Wakili wa Kimataifa wa Usafirishaji wa Majini (IML) Lydia Ngugi akitoa maelezo  kuhusiana na mkataba wa nchi zilizo katika Ukanda wa Magharibi wa Bahari ya Hindi juu ya kutekeleza ya kuepuka madhara ya kimazingira , jijini Dar es Salaam.

Picha za pamoja za Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Kaimu Abdi Mkeyenge na washiriki wa warsha ya kujenga uelewa wa mazingira ya bahari kwa nchi zilio katika Ukanda wa Magharibi wa Bahari ya Hindi, Warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

*Elimu ya mazingira kuendelea kutolewa kwa wadau wa sekta ya usafirishaji

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
NCHI 16 zilizo katika ukanda wa Bahari ya Hindi zimekutana kujadili suala la kupunguza madhara ya mazingira katika bahari na kuendelea kukuza sekta ya usafiri majini.

Sekta ya usafiri majini ni sekta inayochochea uchumi kwa nchi zilizo katika ukanda huo Magharibi wa Bahari ya Hindi.

Akizungumza wakati wa kufungua warsha ya Siku Mbili kwa Washiriki wa nchi hizo katika Ukanda wa Magharibi wa Bahari Hindi uliofanyika jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Kaimu Abdi Mkeyenge amesema kuwa ikiwa wazidhibiti na wanawajibu wa kuangalia sekta ya usafiri majini ina kuwa salama bila kuwepo kwa uharibifu wa mazingira katika bahari pale juhudi za kuendeleza ukuaji wa uchumi wa bluu zinapofanywa.

Amesema warsha ya program ya uelewa wa usafiri wa majini ikiwemo uharibifu wa mazingira unaotokana na vyombo vya usafiri majini na ukuaji wa uchumi wa bluu kwa kuwa na udhibiti endelevu katika kipindi ambacho nchi ziko katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Mkeyenge amesema Tanzania imeombwa kuwa mwenyeji wa warsha baada kuombwa katika Ukanda wa Magharibi wa Bahari ya Hindi.

Aidha, amesema 'Maritime Technology Corporation Centre' ambayo makao makuu kwa Africa yapo Kenya ndio wanaosimamia mkataba wa mzingira ambao unahimiza kuepuka uharibifu wa mazingira uovu kwenye Ukanda huo wa bahari, maziwa na mito.

Mkurugenzi Mkuu huyo amesema ajenda kubwa ni kuangalia matumizi ya teknolojia rafiki na kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana matumizi mazito makubwa ya mafuta na wakati huu Dunia inazungumza jinsi ya kuokoa mazingira oevu.

Amesema, "wadau usafiri wa majini tunajukumu la kutekeleza ajenda ya mazingira salama katika kuhakikisa bahari, maziwa na mito inakuwa salama wakati wote kutokana kuwa ndio usafiri wa uchumi kwa nchi zote duniani."

Mkeyenge amesema warsha hiyo ni muhimu kama ambayo Shirika la Bahari Duniani (IMO) inataka kuwa usafiri njia ya majini unakuwa usafiri salama.

Ameeleza kuwa Tanzania na nchi zilizo ukanda wa Magharibi mwa bahari ya hindi wamekutana na kuendelea kuunganisha nguvu kwa kupeana elimu wakiwemo wamiliki vyombo vya usafiri majini pamoja na watumiaji kuwa makini zaidi ya kutochafua mazingira ya bahari, maziwa na mito.

"Tunawajibu wa kutunza mazingira kwa ajili ya maendeleo ya uchumi endelevu ambapo bila kufanya hivyo uchumi wa bluu hauwezi kufikiwa." Amesema Mkurugenzi Mkuu Mkeyenge.

Amessema TASAC inataka vyombo vya usafiri majini visimwagwe uchafu yakiwemo mafuta kutokana na madhara makubwa yatayofanya viumbe hai na uoto wa asili kutoweka kwenye bahari.

Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa Nairobi Convention wa Shirika la Umoja wa Mataifa linashughulikia Mazingira (UNEP) Dkt. Jared Bosire amesema Sekretarieti ya Nairobi 'Convention' ilipewa amri ya kufanya kazi na wadau wengine ili kuweka mikakati ya kupunguza madhara kwenye mazingira kutokana na ujenzi wa miundombinu ya bahari .

Bosire amesema nchi zinatakiwa kuwa na maendeleo endelevu ambayo hayo maendeleo yanapunguza madhara mazingira ya bahari kwa vizazi vya leo na vijavyo.

Amesema Katika uchumi wa bluu bandari zikijengwa au kupanuliwa kumetolewa muongozo ya wadau kufuata ambao ndio utasaidia kulinda mazingira ya bahari kwa viumbe vilivyopo.

Aidha, amesema mwisho warsha hiyo watakubaliana juu ya kutumia muongozo katika ujenzi wa bandari na upanuzi utaokuwa unapunguza madhara ya mazingira kwenye bahari. 

Nchi 9 zilishiriki mafunzo hayo ambazo ni Kenya, Afrika kusini, Msumbiji, Madagascar, Somalia, Commoro, Shelisheli, Mauritania na Tanzania ikiwa ni nchi mwenyeji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad