HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 13, 2023

DIT Wakamilisha Maboresho ya Mitaala mipya ya fani za Uhandisi

 

Wataalamu wa kuandaa mitaala mpya wa masomo ya uandisi wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Tasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT)
Baadhi ya Washiriki wa kuandaa mitaala mipya ya uandisi wakiwa katika kikao cha pamoja.
Mkuu wa Tasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT),Prof. Presksedis Ndomba akizungumza na Wataalaam.


Na Mwandishiwetu
MKUU wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Profesa Presksedis Marco Ndomba ameipongeza timu ya wadau walioshiriki katika kuandaa na kuboresha mitaala mipya katika fani za Uhandisi Komputa, Mawasiliano angani na Usalama wa Kimtandao katika ngazi ya Uzamili na stashahada ya Mitambo Viwandani.

Ameyasema hayo leo Aprili 12,2023 kwenye warsha ya siku moja iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ASA Kampasi kuu Dar es salaam.

Pia amepongeza juhudi za maandalizi zilizosababisha kupata utaalam kutoka sekta mbalimbali na kupata watu stahiki ambao watasaidia kujadili programu hizo pendekezwa.

“Leo tunazungumzia 'digital skills' ambazo hizi ni programu mahususi kumuwezesha mhitimu kuajirika au kujiajiri na kutatua changamoto zilizopo katika jamii hivyo kwa mchanganyiko wenu huu naamini kabisa maoni yenu na mawazo yenu yatazalisha programu zitakazokidhi mahitaji hayo” amesema Prof. Ndomba.

Aidha, ameelaza kuwa taasisi inasisitiza mafunzo kwa njia ya vitendo ili kuweza kutoa wanafunzi wenye ubora unaokubalika kwenye soko la ajira na hivyo itasaidia DIT kuwa taasisi bora inayoongoza barani Afrika kwenye masuala ya teknolojia

Kwa Upande wa  Mratibu wa Programu hiyo ya kuandaa mitaala Dkt. Fahamuel Mmbaga amesema uboreshaji wa mitaala hiyo utachangia katika kutatua changamoto mbalimbali katika jamii kwa kuchanganya teknolojia mbalimbali ili kurahisisha masuala ya upatikanaji wa huduma.

Pia amesema watatumia utaalamu kujikinga na kupambana na wavamizi wa kimtandao na kutatua changamoto katika jamii.

“Bila ushiriki wa wadau DIT haiwezi kufikia malengo yake ndio maana tumewaalika kuwezesha upatikanaji wa mitaala bora na programu zenye ubora," amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad