HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 25, 2023

TANZANIA KUENDESHA MKUTANO WA NANE WA EAPN KWA KUSHIRIKIANA NA LSF


Mkurugenzi Mtendaji wa Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala akizungumza na waandishi wa habari kuelekea Mkutano wa Nane wa East Africa Philanthropy utakaofanyika Zanzibar kuanzia 28 - 30 Juni 2023. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Foundation for Civil Society (FCS), Francis Kiwanga wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa East Africa Philanthropy Network (EAPN), Evans Okinyi (hayuko pichani) wakati akizungumza na waandishi wa habari kupitia mtandao kuhusu uzinduzi wa tovuti ya usajili wa washiriki kuelekea Mkutano wa Nane wa East Africa Philanthropy utakaofanyika Zanzibar kuanzia 28 - 30 Juni 2023.
Waandishi wa habari wakifuatilia uzinduzi wa tovuti ya usajili wa washiriki Mkutano wa Nane wa East Africa Philanthropy utakaofanyika Zanzibar kuanzia 28 - 30 Juni 2023. Uzinduzi huo umefanywa leo Jijini Dar es Salaam na Afisa Mtendaji Mkuu wa East Africa Philanthropy Network (EAPN), Evans Okinyi wakati alipozungumza na waandishi wa habari kupitia mtandao.
Mkurugenzi Mkuu wa Foundation for Civil Society (FCS), Francis Kiwanga akizungumza na waandishi wa habari kuelekea Mkutano wa Nane wa East Africa Philanthropy utakaofanyika Zanzibar kuanzia 28 - 30 Juni 2023.

TANZANIA kwa kishirikiana na East Africa Philanthropy Network (EAPN),Legal Services Facility (LSF) pamoja na wanachama wengine wanatarajia kuendesha Mkutano wa Nane wa East Africa Philanthropy utafanyika kwa siku mbili mfululizo nchini Tanzania kwenye visiwa vya Zanzibar kuanzia 28 – 30 Juni 2023.


Mkutano wa East Africa Philanthropy ni mkutano wa mwaka unaoendeshwa na East Africa Philanthropy Network (EAPN) ukijumuisha wataalam na taasisi za masuala ya uhisani zaidi ya 300.


Mkutano huo utaambatana na kauli mbiu yake inayosema kuwa Mabadiliko ya Mifumo kihamasisha jitihada za pamoja.


Pia lengo kubwa ni kujadili ubunifu unaoweza kuhamasihsa utekelezaji wa mipango itakayoweza kuleta mabadiliko kwa kuchanganua, kubadilishana uzoefu, kutathimini pamoja na kuunda mpango madhubuti kwa kuzingatia mafanikio na changamoto zilizopo katika sekta ya uhisani.


Akizungumza na vyombo vya habari Jijini Dar es Saalam kupitia njia ya mtandao, Afisa Mtendaji Mkuu wa EAPN, Evans Okinyi, amesema kuwa mkutano huu haulengi kunufaisha sekta ya uhisani peke yake bali unakwenda kuhamasiha mabadiliko ya mifumo ili kuongeza jitihada na kuunda mifumo ya jamii kufanya hisani.


“Haijalishi ni namna gani tunauangalia mkutano huu.


Ukweli ni kwamba muingiliano wa kijamii uliopo katika ulimwengu wa sasa unahitaji jamii inayoweza kufanya kitu ama kuelewa mambo kwa namna nzuri.


Tunalenga pia kuwezesha zaidi wale ambao hawawezi kusema kwa kubadilisha mitazamo yao kifikra ili kuyaangalia mambo ambayo pengine yanaonekana kuwa hayawezekani kuwa yanawezekana,” amesema Okinyi.


Akifafanua zaidi, Mwenyekiti wa Bodi ya EAPN, Jacqueline Asiimwe, amesema kuwa hakuna jawabu la aina moja kuhusu changamoto zilizopo katika sekta ya uhisani, hivyo mkutano huu unalenga kutafuta majawabu kupitia mabadiliko ya mifumo itakayoleta pamoja jitihada za makundi ya wadau mbalimbali ili kuunganisha nguvu ya pamoja kwa kujifunza na kupeana uzoefu kwa ajili ya kufikia mabadiliko yanayohitajika.


“Siku zote kitu ambacho sekta ya uhisani hufurahia ni kupatikana kwa maendeleo, kitu ambacho huonekana kama dalili ya changamoto ambayo tunaiona.


Lakini kwa pamoja tutaweza kuchanganua changamoto zilizopo ikiwemo kukosekana uwajibikaji, matumizi bora ya rasilimali, namna ya kujenga uwezo kupitia ubunifu wa mifumo, na imani isiyobadilika kama njia mojawapo ya kukwepa changamoto zilizopo katika sekta hii,” amesema Jacqueline.


Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala amesema kuwa, mkutano wa mwaka huu umeandaliwa na kamati iliyoundwa na wanachama na wadau wa Mtandao wa EAPN, ambapo LSF inaona fahari kuwa ni mratibu mkuu kutoka nchini Tanzania.


“Mkutano huu ni jukwaa la kubadilishana uzoefu pamoja na kufanya tathmini ya pamoja ili kubuni njia bora za jamii kufanya hisani na kuwekeza kwa ajili jamii na wadau mbalimbali barani Afrika.


Hivyo, nawaomba mashirika yote ya uhisani nchini, sekta binafsi, serikali, CSOs na wadau wengine muhimu wa maendeleo kuungana pamoja katika mkutano huu muhimu,” amesema Ng’wanakilala.


Mkutano wa Nane wa East Africa Philanthropy tayari umefungua tovuti yake kwa ajili ya wadau mbalimbali kufanya usajili wao kupitia www.eaphilanthropyconference.org. Ng’wanakilala pia amepongeza jitihada za Mtandao wa EAPN katika kukuza utamaduni wa kutoa kwa ajili ya jamii kwenye ukanda wa Afrika Mashariki, lakini pia kuamua kuendesha mkutano huu mkubwa nchini Tanzania.


Kuhusu East Africa Philanthropy Network (EAPN)Ilianzishwa mwaka 2003 ikifahamika kama the East Africa Philanthropy Network (EAPN) kabla ya hapo ilifahamika kama East Africa Association of Grant-makers (EAAG), ni mtandao wa taasisi ambazo zina uanachama wa kujitolea.


Mtandao huu unajumuisha taasisi na bodi za udhamini ndani ya Afrika Mashariki kwa lengo la kukuza utamaduni wa kutoa kwa ajili ya jamii.


Wanachama wa EAPN wanatoka katika Bodi za Udhamini katika Familia, Taasisi za Kijamii, Taasisi za Mashirika na Sekta Binafsi, pamoja na Taasisi au Mashirika mbalimbali yanyotoa ruzuku, lakini pia kufanya hisani.


Maono ya EAPN yanalenga kuwa ni jukwaa la pamoja kwa ajili ya kukuza na kuunganisha njia mbalimbali zenye ubunifu katika kuendeleza sekta ya uhisani Afrika Mashariki.


Kwa taarifa zaidi: Evans O. Okinyi,Afisa Mtendaji Mkuu,East Africa Philanthropy Network (EAPN),Koinange Street, Rattansi Educational Trust Building, 4th Floor, Door 1Tel: (+254)-020-3315773; Cell: 0720-340522; Fax: 020 2244470;


Skype: okinyievansWebsite: www.eaphilanthropynetwork.org

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad