HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 27, 2023

RC KUNENGE AMEZINDUA SOKO LA UTETE LENYE VIZIMBA 89

 Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

MKUU wa mkoa wa Pwani, alhaj Abubakar Kunenge amezindua Soko la Utete,lenye vizimba 89 ,ambapo limegharimu kiasi cha sh. milioni 172 .

Akisalimia Wananchi wa Utete wakati wa Uzinduzi huo ,Kunenge ameitaka Halmashauri ya Utete kusimamia upangaji wa wafanyabiashara kwenye Soko hilo ili kuondokana na madalali na kuwa sehemu ya Huduma.

Ameeleza ,Rais Samia Suluhu Hassan, anafanya kazi kubwa kwa Wananchi wa Rufiji ikiwemo Ujenzi wa Miundombinu mbalimbali ili kuwanufaisha wananchi.

Mkuu huyo wa mkoa,amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Rufiji kuanza kupanga Mji wa Utete kwani ni Mji mzuri unaokuwa kwa kasi.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad