HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 1, 2023

UNESCO, Wizara ya Elimu wakutana na wadau kujadili mpango wa elimu kwa maendeleo endelevu kufikia 2030

Na Mwandishi Wetu,


SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kupitia ofisi zake za Dar es Salaam, Kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekutana na wadau mbalimbali katika mkutano wa kisera wa kujadili uandaaji wa mpango mkakati wa elimu kwa Maendeleo Endelevu kwa nchi (ESD 2030).

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, mgeni rasmi, Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bw. Khamis Abdalla Said amesema kuwa mkutano huo una umuhimu wa kipekee katika kusaidia ukuaji wa elimu, maendeleo ya vijana na mabadiliko ya tabia nchi kwa Zanzibar na Tanzania Bara

Ambapo amesema kuwa wataalamu hao kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania, wanashiriki mkutano huo wa kitaifa wenye lengo la kupata muafaka sahihi wa ukuaji wa elimu katika muktadha wa Elimu kwa maendeleo endelevu 2030 (ESD for 2030).

‘’Kuna vipaumbele vilivyowekwa ilikuweza kubadilishwa na katika kuhakikisha sekta ya elimu inakuwa, ikiwemo mafunzo kwa walimu ambao wanamchango mkubwa sana katika ukuaji wa elimu nchini.

Lakini pia masuala ya maendeleo ya vijana na vilevile masuala ya mabadiliko ya tabia nchi.

Washirika hawa watajadili na kupata uelewa hasa masuala haya ya mabadiliko ya elimu, ikiwemo mitaala ya elimu yetu, kubadilisha vipaumbele vya ubora wa elimu ikiwemo mazingira ya walimu.’’

Na kuongeza kuwa, upande wa mabadiliko ya tabia nchi, Tanzania imekuwa na joto kubwa lililoongezeka na kupanda zaidi, huku theluji ya Mlima Kilimanjaro ikiyeyuka, misitu inakatwa, huku bahari ikiwa inaathiri mashamba na baadhi ya maeneo ya Zanzibar hasa upande wa ukanda wa mwambao wa Pwani.

‘’Mkutano huu umewaleta washirika kutoka taasisi za Serikali na zisizo za Kiserikali, taasisi za dini, Vyuo vikuu kusudi kujadili kupata uelewa wa msimamo wa SADC katika malengo ya maendeleo endelevu namba nne kuhusu elimu.

‘’Umuhimu watu hawa wanashiriki katika kusikia kwanza na vipi kila taasisi husika kuweza kujadili na kuja na muafaka katika majadiliano hayo’’ alisema Bw. Khamis Abdalla.

Kwa upande wake, Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Bw. Michel Toto amesema kuwa, ni muhimu kwa Tanzania kushirikiana na mataifa mengine kupitia maendeleo endelevu na masuala yanayojitokeza katika elimu ilikupata majibu sahihi.

Mkutano huo wa siku mbili, una washirikisha wawakilishi kutoka Wizara ya Elimu, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Makamu wa Rais, NEMC, Asasi za kiraia, Taasisi za Elimu, Elimu ya juu, asasi za vijana na washirika wa maendeleo, wanafunzi na wadau wengine wakiwemo Vyombo vya Habari vinavyohusika na elimu kwa maendeleo endelevu.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Khamis Abdulla Said akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kisera wa kujadili uandaaji mpango mkakati wa elimu kwa maendeleo endelevu ulioandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na Serikali unaoendelea jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Bw. Michel Toto akitoa neno la ukaribisho lililoambatana na salamu za shirika hilo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kisera wa kujadili uandaaji mpango mkakati wa elimu kwa maendeleo endelevu ulioandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na Serikali unaoendelea Jijini Dar es Salaam.
Dr Charles Chikunda kutoka UNESCO-ROSA akizungumzia malengo ya mkutano wa kisera wa kujadili uandaaji mpango mkakati wa elimu kwa maendeleo endelevu ulioandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na Serikali unaoendelea Jijini Dar es Salaam.
Dr. Patience Awopegba kutoka UNESCO-ROEA akibainisha vipengele vya mfumo wa kitaifa wa mkakati wa elimu kwa maendeleo endelevu wakati wa mkutano wa kisera wa kujadili uandaaji mpango mkakati wa elimu kwa maendeleo endelevu ulioandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na Serikali unaoendelea Jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Khamis Abdulla Said (katikati) akiwa meza kuu na Mtaalamu wa Program wa Elimu UNESCO-ROEA Dkt. Patience Awopegba (wa kwanza kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Tume ya Taifa ya UNESCO-NATCOM, Bw. Aboud Khamis (wa pili kulia), Kamishna wa elimu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Venance Mawori (wa kwanza kushoto) pamoja Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Bw. Michel Toto (wa pili kushoto) wakati ufunguzi wa mkutano wa kisera wa kujadili uandaaji mpango mkakati wa elimu kwa maendeleo endelevu ulioandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na Serikali unaoendelea jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa mkutano wa kisera wa kujadili uandaaji mpango mkakati wa elimu kwa maendeleo endelevu Bi. Fatma Mrope kutoka Tume ya Taifa ya UNESCO (NATCOM) akifungua majadiliano wakati wa mkutano huo uliaondaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na Serikali unaoendelea Jijini Dar es Salaam.
Mdau wa Maendeleo anayeshughulikia Elimu Bi. Patricia Viala (katikati)kutoka Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) akichangia mada wakati wa mkutano wa kisera wa kujadili uandaaji mpango mkakati wa elimu kwa maendeleo endelevu ulioandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na Serikali unaoendelea jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalosguhulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Faith Shayo na kulia ni Bi. Jennifer Kotta kutoka ofisi za Unesco nchini.
Meneja Idara ya Utafiti, Ubunifu na Uchambuzi wa Sera kutoka Haki Elimu, Bw. Makumba Mwemezi akitoa maoni wakati wa mkutano wa kisera wa kujadili uandaaji mpango mkakati wa elimu kwa maendeleo endelevu ulioandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na Serikali unaoendelea jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Elimu Zanzibar, Bw. Abdallah Mohamed Musa akichangia mada wakati wa majadiliano kwenye mkutano wa kisera wa kujadili uandaaji mpango mkakati wa elimu kwa maendeleo endelevu ulioandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na Serikali unaoendelea jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Kisera wa kujadili uandaaji mpango mkakati wa elimu kwa maendeleo endelevu, wakifuatilia ufunguzi wa mkutano huo wa siku mbili, ulioanza mapema leo Jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bw. Khamis Abdulla Said (kulia) akibadilishana mawazo na Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalosguhulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi. Faith Shayo (kushoto) wakati wa mkutano wa kisera wa kujadili uandaaji mpango mkakati wa elimu kwa maendeleo endelevu ulioandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na Serikali unaondelea jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bw. Khamis Abdalla Said akiwa katika picha ya pamoja na makundi mbalimbali wakiwemo wadau wa maendeleo walioshiriki mkutano wa kisera wa kujadili uandaaji mpango mkakati wa elimu kwa maendeleo endelevu ulioandaliwa na UNESCO kwa kushirikiana na Serikali unaondelea jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad