HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 25, 2023

TANROADS IMEWATAKA WATUMISHI WAKE KUTENGA MUDA WA MAZOEZI

  


Meneja wa TANROADS Mkoa Morogoro Mhandisi Alinanuswe Kyamba akizungumza na watumishi walioshiriki wa bonaza la michezo ( hawapo pichani) lililofanyika mjini Morogoro.
Michezo mbalimbali ikiendelea.

Na Farida Mangube, Morogoro
WAKALA wa barabara Tanzania (TANROADS) imewataka watumishi wake nchini kutumia muda mwingi kufanya kazi huku wakitenga muda wa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya ya mwili kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.

Akifungua bonaza la wafanyakazi wa TANROADS kutoka mikoa 9 Mkurugenzi wa huduma za uendeshaji kutoka makao makuu Mhandisi Emil Mkaki alisema mazoezi hupunguza kasi ya magonjwa ya kuambukiza ambayo Rais Samia Suluhu Hassan kila mara amekuwa akisisitiza kufanya mazoezi.

Alisema TANROADS imeweka utaratibu kwa kila mkoa kufanya mazoezi angalau mara mbili kila wiki kwa wafanyakazi wake na kwamba wakitumia vyema muda huo itasaidia kuwaweka vyema kiafya na kujikuta wakiwa imara hata katika utendaji kazi zao.

Alisema lengo la bonaza Hilo ni kutekeleza maagizo ya serikali kwamba kila Taasisi idumishe michezo ili kupunguza magonjwa yasiyoambukiza ambayo yamekuwa yakisumbua kwa jamii na kwamba bonanza hilo pia huleta mshikamano wa wafanyakazi na kubadilishana mawazo.

Naye Meneja wa TANROADS mkoani Morogoro Mhandisi Alinanuswe Kyamba aliwasisitiza watumishi kuzingatia bonanza hilo sababu linasaidia kujenga umoja baina ya wafanyakazi na kutunza afya za watumishi.

Alisema bonaza hilo linashirikisha wafanyakazi zaidi ya 500 wakishiriki michezo ya mpira wa miguu, kuvuta kamba, mpira wa pete, riadha, sambamba na michezo ya jadi ikiwemo kufukuza kuku, kukimbia kwenye magunia, bao la kete na draft.

Naye Mmoja wa washiriki wa bonanza hilo Mfanyakazi wa TANROADS Iringa Dickson Mganga alipongeza juhudi za kuanzishwa bonanza hilo ambalo linawaweka vyema kiafya sababu zamani walikuwa hata wakishindwa kukimbia kwa umbali mrefu jambo ambalo ni tofauti kwa sasa.

Naye Rehema Mdime kutoka Morogoro alisema bonanza hilo limekuwa chachu kwao ya kuwafanya kuwa na morali ya kujiandaa vyema katika michezo ijayo baada ya kushindwa katika mpira wa pete baina ya yao na Mtwara.

TANROADS ina mpango wa kupanua wigo wa michezo kwa kufanya bonaza nchi nzima ili kuwakutanisha watumishi na kufanya tamaduni hiyo kuendelea kuwepo kila mwaka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad