HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 18, 2023

Serikali yawaonya wanaoomba rushwa ya ngono mashuleni na vyuoni

Wabunge wa kamati ya kudumu ya bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, wakisalimiana na uongozi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili Muhimbili kitengo cha Mloganzila ( MUHAS) Kibaha mkoani Pwani walipowasili kwenye ziara yao chuoni hapo. SERIKALI imesema itahakikisha inawalinda watoto wote wa kike wanaosoma Sekondari na wale wa vyuoni dhidi ya wahadhiri na 'mabazazi' watakaobainika kuomba rushwa ya ngono kwa kiwachukulia hatua kali za kisheria.


Hivyo wanafunzi hao wametakiwa kutoa taarifa kwa mamlaka pindi wanapotakiwa kutoa rushwa hiyo ya ngono.

Wahadhiri na walimu watakaobainika kuomba rushwa ya ngono kwa wanafunzi kike wa shule za sekondari na vyuoni hatutawafumbia macho, tutahakikisha pindi wakibainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ameyasema hayo Machi 17,2023 wakati ya ziara ya kamati ya kudumu ya bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo katika Chuo Kikuu Muhimbili kitengo cha Mloganzila ( MUHASI) Kibaha mkoani Pwani.

Alisema kuwa iko wazi kuwa idadi ya wanafunzi wa masomo ya sayansi nchini bado ndogo lakini bado wanafanya uchunguzi kubaini kama tatizo hilo linasababishwa na wao kuombwa rushwa ya ngono na hivyo kuwafanya kuogopa kuchukua masomo ya Sayasi au la.

Tumekuwa tukichukua hatua za kimya kimya kwa watumishi wanaojihusisha na tabia hizo... tunaomba wasichana wote kuripoti kwa mamlaka kama wanaombwa rushwa ya ngono kwani hii itakusaidia kuwabaini mabazazi ambao wanataka kukakatisha ndoto zao," amesema Profesa Mkenda.

Amesema kuwa, masomo ya tiba yamekuwa na changamoto mbali mbali kwani wanafunzi wanapofeli somo moja, hawezi kuendelea na masomo kwa mwaka unaofuata kwa sababu wanahitaji wataalamu wazuri wa tiba.

Profesa Mkenda ameeleza hayo kufuatia swali kutoka kwa Mjumbe wa Kamati ya hiyo Anastasia Wambura kuuliza sababu ya kuwepo kwa wanafunzi wachache wasichana wanaosomea shahada ya awali ukilinganisha na wanaume.

Wambura alisema kuwa rushwa ya ngono imekuwa ikiwafanya wasichana wengi kuogopa kujiunga na masomo ya sayansi kutokana na kupewa taarifa na marafiki zao kuhusu ugumu wa masomo hayo.

Alisema kuwa baadhi ya walimu na wahadhiri wamekuwa wakichafua taswira ya vyuo vikuu hivyo anapaswa kuchukuliwa hatua ili wasichana waone kuendelea na masomo ni muhimu.

"Vyuo viangalie suala la rushwa ya ngono kwa wasichana kwani utaona wasichana wanaojiunga na vyuo vikuu vya sayansi na mengine ni wachache kuliko wavulana. Sababu wameshaambiwa na ndugu zao kwamba masomo ya vyuo ni magumu na ili wafaulu, watapaswa kutoa rushwa ya ngono,'' alieleza Wambura.

Pia alisema idadi ya wanafunzi wa kike katika masomo ya shahada ya uzamili wamekuwa wengi ikilinganishwa na wanaume kwa sababu wamebaini kwamba masomo ya sayansi na tiba si magumu kama inavyodaiwa na tayari wanakuwa wamejitambua.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Kitila Mkumbo imeshauri serikali kuhakikisha inakamilisha mradi wa awamu ya pili ya ujenzi wa Kituo cha Umahiri wa Magonjwa ya Moyo Mloganzila ili wanafunzi waweze kupata mafunzo kwa vitendo na kuongeza idadi ya madaktari wa kutibu ugonjwa wa Moyo.

"Tunaishauri serikali kuhakikisha inajenga hospitali kwa ajili ya wanafunzi kupata mafunzo kwa vitendo ili kubobea katika kutibu magonjwa ya moyo,'' amesisitiza Profesa Mkumbo

Amesema kuwa wamebaini kuwa vyuo vya Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas) vimekuwa vikitoa mafunzo yatakayowawezesha wanafunzi wao kujitegemea na kutoa huduma bora.
Wabunge wa kamati ya kudumu ya bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, wakimsikiliza mhadhiri Msaidizi, Dkt. Eka Kisali kutoka maabara ya afya wakati walipotembelea  katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili ( Muhimbili kitengo cha Mloganzila ( MUHAS) Kibaha mkoani Pwani. Machi, 17 2023.
Waziri wa Elimu,  Sayansi,na Teknolojia Profesa Adolph Mkenda akizungumza na wabunge wa kamati ya kudumu ya bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo,  pamojan na baadhi ya vongozi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili Muhimbili  ( MUHAS) wakati wa ziara ya  ya bunge chuoni hapo Machi 17, 2023.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad