HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 13, 2023

SAFARI YA DKT SAMIA NA MAPINDUZI MAKUBWA KWENYE SEKTA YA ELIMU KIBAHA MJI

 


Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
NI takribani siku 730 zinazobeba Miezi 24 sawa na saa 17,520 ,sawa na miaka miwili ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kazini baada ya kifo cha Hayat Dkt.John Magufuli kututoka, na kuacha majonzi kwa Taifa, kumpoteza Rais akiwa madarakani.


Hii ni historia ambayo hatuitamani iliyotokea Machi 17,2021 ,licha ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwakuwa halipangalo halipingiki.


Tarehe 19 Machi,2021 ilikuwa ni mwanzo wa safari mpya ya Dkt.Samia baada ya kuapishwa na kula kiapo na kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama.


Siku zinakwenda ,safari ni hatua!Sasa anatarajia kutimiza miaka miwili hapo Machi 19,2023, na kwa hakika anaonyesha namna alivyomchapakazi na matunda yanaonekana katika nyanja zote hususan elimu.


Halmashauri ya Mji Kibaha ,ni miongoni mwa Halmashauri ambayo imesafiri na Rais Samia kwenye kipindi chote hatua kwa hatua ,na kunufaika na matunda ya ya safari yake ,Na tuangazie namna Dkt.Samia alivyoangazia Elimu Sekondari na kuibadili taswira machoni pa wengi.


Ni ukweli usiopingika kuwa ameng'amua usemi wa wahenga usema ulimu ni ufunguo wa Maisha,Ufunguo umetua Kibaha na kufungua kwa kutatua changamoto za kielimu na hatimae kuboresha Mazingira ya elimu.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha ,Mshamu Munde anaeleza kuwa tayari sh.bilioni 3,081,000,000.00 zimetua Kibaha Mji na kutumika kuiboresha sekta ya Elimu Sekondari.


"Madarasa 103 yenye thamani ya Sh.bilioni 2,080,000,000.00 yamekamilika,yanatumika kuboresha uwezo wa ujifunzaji kwa wanafunzi kuinua Kiwango cha taaluma."


Aidha,jumla ya sh.milioni 200,000,000 kuikarabati shule ya Sekondari Tumbi ili kuirudisha kwenye hali ya usasa.


Dkt.Samia amedhamiria makubwa kwenye sekta ya Elimu Sekondari, Serikali ndani ya kipindi cha miaka miwili imepitisha kiasi cha sh.milioni 470,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Viziwaziwa kupitia mradi wa SEQUIP.


"Tayari miundombinu ya Madarasa,maabara,majengo ya utawala,maktaba,TEHAMA na mahitaji mengine yamekamilika, shule ipo mguu sawa kuwapokea wanafunzi na walimu tayari kwa kazi,Kazi Moja tu,masomo kuwapa wanafunzi maarifa mapya"anasema Munde.


Munde anafafanua,ni wakati huohuo milioni 531,000,000.00 zimetumika kujenga miundombinu mingine mathalani;bwalo,matundu ya vyoo,majengo ya utawala,ofisi za walimu na maabara ili kuweka Mazingira wezeshi ya kutolea Elimu.


Nickson Simon,Mkuu wa Wilaya ya Kibaha anampongeza Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili madarakani na kumshukuru kwa kutoa fedha nyingi Kibaha kuimarisha Sekta ya Elimu .


Anaahidi kuzidi kumsaidia kusimamia maendeleo ya Mji huo na kwamba anawataka watendaji kujituma , kufanya kazi zinazoleta matokea chanya kwa wananchi.


Nae ofisa elimu sekondari, Rosemary Mary Msasi anaelezea, majengo hayo yamesadia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto za majengo na miundombinu na anaahidi kuongeza usimamizi wa karibu ili yatumike kwa kipindi kirefu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad