HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 26, 2023

PASS YAANZISHA KAMPUNI TANZU, KUPANUA WIGO WA HUDUMA ZAKE

 



TAASISI ya kusaidia sekta binafsi ya kilimo ( PASS) imeanzisha kampeni tanzu iitwayo Pass leasing ili kupanua wigo wa huduma zake ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo kwa asilimia 80 ya zana za kilimo na viwanda bila dhamana kwa kushirikiana na wasambazaji wa zana hizo.

Mkurugenzi wa Masoko wa PASS, Adam Kamanda ametoa taarifa hiyo kwenye mkutano wa mashauriano na wadau wa sekta ya kilimo wa kuhamasisha uzalishaji unaozingatia ukuaji wa kijani shirikishi uliofanyika pia mkoani tabora.

Kamanda ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa PASS, Yohana Kaduma amesema, kwa miaka 23 iliyopita PASS imewanufaisha wajasiliamali milioni 3.4 ambao wametoa ajira milioni 2.7 kati yao asilimia 51 ni Wanawake nchini.

Amesema kwa kipindi hicho benki 14 zilishirikiana na taasisi hiyo na kutoa mikopo yenye thamani ya trioni 1.3 katika 66,077 nchi mzima ambazo zimesaidia kubadilisha hali ya maisha ya watanzania wakiwemo wajasiliamali mali na waajiriwa hao na familia zao.

Kamanda amesema kwa kipindi hicho PASS imekuwa daraja muhimu sana katika kuwawezesha wakulima, wavuvi, wadau wa sekta ya misitu, wafugaji na wajasiliamali wengine kwenye mnyororo mzima wa thamani.

Mkutano huo ulienda sanjari na uzinduzi wa kampeni ya kujanisha maisha na programu ya ukuaji wa kijani katika maisha kwa kanda za kaskazini na magharibi.

Akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurudim Babu ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kisare Makori aliipongeza PASS kwa kuja na mpango wa kukuza uchumi kupitia ajenda ya ukuaji wa kijani shirikishi kama njia bora ya kuchochea kilimo endelevu

Kwa upande wa Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Tabora, Ezekiel Mwansasu amezitaka taasisi za fedha kuwa karibu zaidi na PASS ili kufanikisha mipango yake na kuwakomboa watanzania wenye kipato cha chini.

Miongoni mwa walionufaika na taasisi hiyo, Jeremia Ayo wa kijiji cha Mbunguni wilaya ya Arumeru mkoani Arusha amesema wamenufaika na kubadilisha mfumo wao wa maisha kwa miaka 23 iliyopita.

Ayo amesema katika kikundi chao wapo wanufaika zaidi 1000 ambao wameweza kujenga nyumba bora za kuishi, kuanzisha miradi ya kiuchumi na kuwasomesha watoto wao hadi Vyuo Vikuu na Vyuo vya kati na baadhi yao sasa wanajitegemea.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad