HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 2, 2023

MAMLAKA YA HALI YA HEWA YATOA ANGALIZO LA MVUA KUBWA MIKOA SITA

 

MAMLAKA ya Hali ya Hewa (nchini TMA) imetoa angalizo la uwepo wa mvua kubwa siku moja ya kesho Machi 3, 2023 kwa mikoa sita na upepo mkali kwa siku mbili, kesho na kesho kutwa Machi 4,2023 katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Katika taarifa iliyotolewa na TMA leo Machi 2, 2023  ilitoa angalizo hilo la mvua kubwa katika mikoa ya Mara, Simiyu, Shinyanga, Mwanza, Dodoma na Singida, pia uwepo wa upepo mkali unaofikia kilometa 40 kwa saa maeneo ya pwani ya Kusini mwa bahari, mikoa ya Lindi na Mtwara .

Athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa shughuli za uchumi na usafirishaji na pia kuathirika kwa baadhi ya shughuli za uvuvi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad