HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 30, 2023

MAJLIS AL-MAARIFA YAUNGA MKONO HARAKATI ZA UPATIKANAJI DAMU SALAMA ZANZIBAR

 Na Mwashungi Tahir - Maelezo Zanzibar. 22-3-2023

TAASISI ya Majlis al- Marifa Islamia imekabidhi vifaa vya kinga katika kitengo cha uchangiaji damu salama, vitakavyo saidia katika harakati za uchangiaji damu.

Hayo ameyasema Mwenyekiti wa Taasisi ya Majlis al-Marifa Tahir Khatib Tahir wakati akikabidhi msaada huo huko katika Kitengo cha damu salama. Sebleni.

Mwenyekiti huyo amesema jumuiya yao inajipanga kutoa misaada hiyo kila baada ya miezi sita ili wafanyakazi waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi .

Aidha alisema uwamuzi wa kupeleka msaada huo katika kituo hicho ni kwa nia ya kuengeza nguvu katika harakati za uwekaji wa damu salama .

“Damu ni muhimu na inahitajika katika Maisha ya kila siku, kila mtu ni muhitaji wa damu wakati wowote hivyo ni vyema kuelekeza nguvu zetu katika kusaidia kitengo hicho,” alisema Mwenyekiti huyo.

Alieleza kuwa Taasisi yao iko katika kusaidia watu wenye mazingira magumu wakiwemo mayatima pamoja na waliyopata maafa .

Alifahamisha lengo la misaada hiyo ni kuwakinga wafanyakazi ili kujinusuru na maradhi yanayoambukiza wakati wa ufanyaji wa kazi zao na kuhakikisha wanaishi katika hali ya usalama.

Pia alifafanua kuwa Taasisi hiyo kwa kushirikiana na serikali husaidia jamii iwapo kutatotokea maradhi ya mripuko sambamba na kusaidia uchimbaji wa visima katika misikiti mbali mbali .

Nao wafanyakazi wa kitengo hicho wameishukuru Taasisi hiyo kwa kuwapatia msaada huo utakaowarahisishia majukumu yao ya kila siku.

Jumla ya shilingi laki nane zimetumika katika kununulia vifaa hivyo ikiwemo barakoa, Spiriti, bendeji, na pamba .
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Majlis Al-Maarifa Islamiya Tahir Khatib Tahir(katikati) akimkabidhi Meneja wa Progaramu ya Damu Salama Dkt. Masud Ali Masud(wakwanza kushoto) msaada wa Vifaa kinga vyenye thamani ya shilingi Laki nane,huko Afisi za Damu Salama Sebleni Zanzibar Machi 22,2023.
PICHA NO.0551:-Afisa Uhusiano kituo cha Damu Salama Usi Bakar Mohammed akitoa neno la shukrani kwa Taasisi ya Majlis Al-Maarifa Islamiya mara baada yakupokea msaada wa Vifaa kinga vyenye thamani ya shilingi Laki nane kutoka kwa Taasisi hiyo, huko Afisi za Damu Salama Sebleni Zanzibar.Machi 22,2023.PICHA NA FAUZIA MUSSA MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad