HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 18, 2023

GF Trucks & Equipment’s Ltd yawapiga msasa wachimbaji madini Chunya.

  


Wakati maonyesho ya madini yakifikia ukingoni kampuni ya uuzaji wa mitambo ya magari ya mizigo Gf Trucks & Equipment iliandaa semina elekezi kwa ajili ya wachimbaji wa madini na viongozi wa chama cha wachimbaji madini yenye lengo la kuwajengea uwezo

Maonyesho hayo ambayo kwa mara ya kwanza yamefanyika wilayani Chunya mkoani Mbeya, yamefungua fursa kwa wafanyabiashara katika sekta hiyo ya madini kukutana na kuweza kubadilishana uzoefu kwani katika maonesho hayo ya makampuni tofauti nchini yalishiriki na kubadilishana uzoefu na wachimbaji hao.

Akizungumza wakati wa semina elekezi Meneja Masoko na Mawasiliano wa kampuni ya GF Trucks ,Smart Deus alisema wachimbaji wengi wanauwezo wa kununua na hata kukodisha mitambo ya huduma ambayo inapatikana katika kampuni yetu ya GF lakini tatizo kubwa hawana uelewa wa kutosha katika uendeshaji kazi, ambayo anaachiwa opareta wa mashine wakati mwingine anaweza kumuongopea bosi kuwa Mtambo unatumia mafuta mengi kumbe ni si kweli, sasa kupitia semina hii tumewaeleza namna bora ya kuitunza mitambo ili iweze kudumu muda mrefu na kuepukana na matatizo yanayoweza kuzuilika

Gf kwa sasa imefungua kiwanda cha kutengeneza maroli ya GFA kilichopo Kibaha mkoani Pwani kwa kutanua na kutumia magari ya FAW unaliongezea Taifa fedha, kwani magari hayo yanatengenezwa nchini kwetu na sisi tunajivunia cha kwetu.

Pia GF hivi karibuni itafungua ofisi (yadi) katika mkoa wa Mbeya ili kuwasogezea huduma jirani wachimbaji kutoka ukanda wa nyanda za juu kusini kwa hiyo wateja wa Njombe,Chunya na Songwe wakae mkao wa kula wa kusogezewa huduma jirani hii ikiwa ni kutii maagizo ya mkuu wa mkoa wa Mbeya aliyetutaka kusogeza jirani huduma zetu.


GF pia ni wauzaji wa mashine za XCMG,AJAX, pamoja na maroli ya mizigo ya FAW na HONGYAN.


Akitoa neno la shukrani Mwenyekiti wa Chama Cha Wachimbaji Madini mkoani Mbeya (Mberema) Leonard Manyesha alisema anawashukuru GF kwa kuweza kuwapa semina elekezi juu ya namna bora ya kutunza na kuisimamia mitambo yao katika shughuli za uchimbaji iliiweze kudumu kwa wakati na kuepuka kupata hasara zinazoweza kuzuilika Pia alisema wamefurahia kupata utaratibu rafiki kwa kuweza kukopa mmitambo hiyo kupitia mmoja ya benki kwa kutimiza mashari nafuu ambayo dhamana itakuwa mtambo wenyewe.

 Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini mkoa wa Mbeya(Mberema) ,Leonard Manyesha  akipokea zawadi ya vifaa kutoka kwa Meneja Masoko na Mawasiliano GF Trucks & Equipment , Smart Deus kwa ajili ya kujikinga na vumbi pamoja na jua wawapo mgodini mara baada ya semina elekezi iliyooendeshwa na kampuni ya Gf wakati wa maonyeshobya madini yaliofanyika Chunya mkoani Mbeya.

Afisa  Mauzo wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd ,  Peter  William akiwaezea ubora wa magari ya mizigo ya FAW  kwa ajili ya matumizi ya  migodini  wakati wa semina elekezi iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya Viongozi  na wachimbaji wa madini  wakati wa maonyesho ya  Teknolojia ya Madini yaliofanyika  Chunya mkoani Mbeya
Meneja Masoko na Mawasiliano GF Trucks & Equipment, Smart Deus na Afisa Mauzo wa kampuni hiyo Peter Willium  wakijadiliana jambo na viongozi wa  Chama   cha wachimbaji madini mkoa wa Mbeya (MBEREMA), upande wa kulia wakati wa semina ya namna bora wa kutumia mitambo  ya XCMG na magari ya FAW kwa wachimbaji iliyofanyika Chunya mkoani Mbeya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad