HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 15, 2023

BRAC WAENDELEA NA UTARATIBU WA KUWAWEZESHA KIUCHUMI WATOTO WA KIKE

 



WANAWAKE wametakiwa kutumia fursa wanazoziona , kutokatishwa tamaa na maneno ya watu na kushindwa kushiriki katika masuala ya kimaendeleo.

Taasisi isiyo ya kiserikali ya Brac Tanzania imeendelea kushiriki katika maendeleo na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kumuwezesha mtoto wa kike kujiinua kiuchumi.

Meneja wa Vijana na Uwezeshaji wanawake kutoka BRAC Upendo Daud amesema wamekuwa na miradi mingi ya kuwawezesha mabinti wa kike kuweza kupata ujuzi sambamba na kuwapatia elimu ya ujasiriamali.

Upendo amesema, Brac imekuwa na miradi mingi tofauti ya kusaidia wakina mama na wasichana inayojulikana kama Goal ambapo kwa sasa inaendelea katika maeneo ya Buguruni na Vingunguti.

Amesema, mbali na mradi wa Goal kuna mradi wa AIM ambapo rasmi ilianza rasm2022 na inapatikana pia katika kikoa mitano tofauti nchini.

"Lengo la Brac ni Kumuwezesha mtoto wa kike aweze kujisimamia na kuwapa ujuzi na kuwawezesha kiuchumi na kwa sasa kuna takrobani Wasichana 200 ambao wapo katika mafunzo ya kuwawezeshwa kupitia Veta na Club mbalimbali,"

"Jumla ya wasichana 135 wapo Chuo cha Veta na wengine wapo kwenye hizo Club zinazopatikana katika maeneo mbalimbali ambapo Brac inatafuta eneo inalipia nyumba na kupata mafunzo hayo na wengi wao wanaokua katika hizi Club ni Wanafunzi," amesema

Upendo ameongeza kuwa kwa mwaka 2022 wasichana zaidi ya 400 walipata mafunzo hayo na kuhitimu na wengine kuwezeshwa kiuchumi kwa kuwapatia vifaa vya kufanyia kazi.

Aidha, Brac Tanzania imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo kwa kushiriki katika miradi ya uwezeshaji wakina mama nchini na kuwahamasisha wanawake kujiunga na Vikundi kwani vimekuwa vinawasaidia katika kujiinua kiuchumi.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad