HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 20, 2023

Boeing 767-300F yenye uwezo wa kubeba tani 54 kuwasili nchini Aprili, 2023

 

Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu na Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi wakionesha mfano wa picha ya Ndege ya mizigo itakayo kuja Aprili, 2023 Kwaajili kutatua changamoto ya usafirishaji wa mizigo nchini.

SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL) inatarajia kupokea ndege ya kwanza ya mizigo aina ya Boeing 767-300F yenye uwezo wa kubeba tani 54 Aprili, 2023 ambayo itatua changamoto ya usafirishaji mizigo hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu wakati akizungumza na wadau wa Usafirishaji Mizigo, wafanyabiashara pamoja na wawakilishi kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali jijini la Dar es Salaam leo Machi 20, 2023 amesema kuwa ndege hiyo itaweka historia Afrika Mashariki na nchi Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, (SADC).

Mchechu amesema kuwa awali ATCL ilikuwa ikitumia ndege abiria kusafirisha mizigo zilikuwa na uwezo wa kubeba tani chache ukilinganisha na uhitaji wa soko la mizigo.

Pia amewataka ATCL kuendelea kuimarisha ushirikiano na wadau wao ili kutatua changamoto zinazokwamisha ufanisi wa biashara hii pamoja na kusimamia maslahi mapana ya pande zote yaani wadau na Serikali.

“Ofisi yangu ina wajibu wa kusimamia mashirika yote nchini likiwemo ATCL ili kuhakikisha yanajiendesha kimkakati kupitia uwekezaji mkubwa unaofanya na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.” Amesema

Akizungumzia mahitaji ya soko duniani amesema kwa mujibu wa Ripoti ya Soko la Usafirishaji wa Mizigo ya 2023, ukubwa wa soko la mizigo limekua kutoka $191.01 bilioni mwaka 2022 kufikia $199.09 bilioni kwa mwaka 2023 kwa kiwango cha ukuaji wa kila mwaka (CAGR) cha 4.2% na ukubwa wa soko la usambazaji wa mizigo unatarajiwa kukua hadi $224.78 bilioni mwaka 2027 kwa kiwango cha CAGR ya 3.1%.

Kwa Upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi amesema kuwa ATCL inajivunia kwa kutoa huduma za uhakika, salama na endelevu za ubora wa juu duniani kote.

Amesema kuwa kupitia mkutano huo watachukua maoni kutoka kwa wadau wa usafirishaji mizigo yatakayowezesha kuondoa kero na urasimu kwenye biashara ya Mizigo.

“Yapo mambo yanayotakiwa kufanyiwa maboresho hasa yenye urasimu lakini yapo ambayo ni ufuataji wa sharia za kulinda usalama wa uendeshaji wa biashara hii. Katika kikao hiki wadau watajadili na kukubaliana masuala ya kufanyiwa kazi na kuweka malengo. Lakini pia tutaambizana ukweli kwa wafanyabiashara ambao hawafuati sharia ambazo kimsingi ni kwa faida ya pande zote mbili,” alisema.Imetolewa na Kitengo cha Uhusiano kwa UmmaShirika la Ndege Tanzania (ATCL)." Amesema Matindi

Kwa sasa ATCL ina ndege 12 na imefanikiwa kupanua mtandao wake hadi kufikia vituo 14 vya safari za kitaifa, 8 za kikanda na 2 za mabara.

Kwa Upande wa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni inayosafirisha mizigo ya maua, matunda, viungo na mbegu, Amani Temu ameishukuru serikali kwa kusikia kilio chao na inaleta ndege ya mizigo.

“Suruhisho la changamoto tuliyokuwa nayo ni hii ndege inayokuja, kwa sisi wadau wa sekta ya usafirishaji tunategemea kuitumi kutokana na wingi wa mizigo na ukuaji wa sekta, tutatumia ndege hii ya mizigo.”

Awali amesema kuwa kulikuwa na changamoto ya ukosekanaji wa nafasi za kusafirisha mizigo kwenye ndege hasa katika kipindi ambacho kunakuwa hakuna abiria wengi kwa sababu tulikuwa tunategemea ndege za abiria na upatikanaji wa nafasi ya mizigo unakuwa mdogo.
Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu akizungumza na wadau wa sekta ya usafirishaji mizigo leo Machi 20, 2023 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Machi 20, 2023 wakati wa kongamano la wadau wa usafishaji mizigo.
Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Machi 20, 2023 wakati wa kongamano la wadau wa usafishaji mizigo.
Upande wa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni inayosafirisha mizigo ya maua, matunda, viungo na mbegu, Amani Temu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Machi 20, 2023.
Mmoja ya wadau wa usafirishaji Mizigo kutoka Zanzibar akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Machi 20, 2023.
Baadhi ya wadau wa usafirishaji wakiwa kwenye kongamano lililofanyika leo Machi 20, 2023 jijini Dar es Salaam.

Picha ya Pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad