HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 14, 2023

Viongozi na Wananchi wa Wilaya ya Longido wapongeza ujenzi wa chuo cha VETA

Mkuu wa Chuo cha VETA  Arusha Bongantabona Deusdedit Mrefu akizugumza kuhusiana  na ujenzi huo wa Chuo cha VETA Longido kilichojengwa na Chuo cha VETA Arusha kwa mfumo wa  Force Account.

 

Mwalimu wa Chuo cha VETA Arusha George Mosha akizungumza kuhusiana na ushiriki wa wananchi wa Wilaya ya Longido walivyoshiriki ujenzi wa Chuo cha VETA Longido.
Moja ya Darasa likiwa lina samani kwenye Chuo cga VETA Longido mkoani Arusha.
Jengo la Utawala wa Chuo cha VETA Longido kinachotarajia kuanza mwezi Aprili kwa Kozi fupi.
Mwananchi wa Kijiji cha Orbomba Maria Mollel akizungumza kuhusiana na fursa kuhusiana fursa za wasichana wa kimasai kupata ujuzi katika Chuo cha VETA Longido
Mwenyekiti wa Kijiji cha Oltepesi wilayani Longido Senjoi Lendia akizungumza kuhusiana na fursa ya vijana wa Longido kutokana na ujenzi wa Chuo cha VETA wilayani  Longido.
Diwani wa Kata ya Orbomba wilayani Longido  Ndiono Nangeresa Mollel akizungumza na waandishi habari kuhusiana na Ujenzi wa Chuo cha VETA katika Wilaya ya Longido.


*Waahidi kupeleka vijana kusoma kwani mifugo hakuna

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV, Longido
WANANCHI na Viongozi wa Wilaya ya Longido wamepongeza Serikali kupitia kwa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kwa kujenga Chuo cha VETA Longido kwani vijana wengi wanahitaji mafunzo hayo kwa ajili ya kuja kutumikia wilaya hiyo katika nyanja za ufundi mbalimbali

Wakizungumza na Michuzi Blog katika Chuo hicho Diwani wa Kata wa Olbomba Ndiono Mollel amesema kuwa Ujenzi wa Chuo hicho umekuja katika wakati mwafaka kwani wanahitaji vijana waende kusoma kutokana na mahitaji ya wilaya kuwa na mafundi na wataalam wa mifugo.

Amesema kuwa serikali imefanya kazi kubwa hivyo wanaomba Chuo kifunguliwe mapema kutokana na nguvu kubwa uliyowekwa katika ujenzi huo na kutaka kuona faida yake ni pale vijana wameingia na kuanza kusoma katika Chuo hicho.

Mollel amesema kuwa maisha ya sasa yanaenda kisasa hawawezi kuwa kazi za ufundi zinafanywa na watu wa Wilaya nyingine wakati ni fursa kwa vijana wa Wilaya ya Longido kupata ufundi kwani kunahitaji wajenzi ambao watafanya wananchi kuwa nyumba za kisasa ,Mafundi Umeme kuwaungashia wananchi,pamoja na mafundi wa magari na pikipiki

Aidha Diwani huyo amesema kuwa Wilaya ya Longido kuna shughuli za Utalii hivyo VETA iangalie kuweka kozi hiyo ambapo itasaidia vijana wilaya hiyo kushiriki shughuli za utalii na kujiongezea kipato kutokana na watalii wanaoingia katika wilaya.

Mwenyekiti wa Kijiji Oltepesi wilayani Logindo Senjoi Lendia amesema kuwa ujenzi wa Chuo kuna mwanga unaonekana kwa wilaya hiyo kutokana maisha ya sasa yanakewenda kisasa kwa kuhitaji mafundi ambao wamesomea na kutofautisha na miaka nyuma.

Amesema Serikali imejenga Chuo kazi ni kwao kupeleka vijana na hakutakuwa na maana ya kujenga chuo hicho kwani vijana wa Longido wamelengwa kupatiwa ufundi na ujuzi wa kuendeleza maisha yao.

Mkazi wa Kijiji cha Orbomba Maria Mollel amesema kuwa Wamasai sasa tumebadilika hivyo elimu inahitajika kwani mifugo inakufa lakini elimu haifi hiyo wanaomba Serikali kupeleka elimu ya watu wazima ili wasome.

Amesema kuwa Rais Dkt.Samia Hassan Suluhu amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wake wanapata elimu huvyo kwa kabila la Wamasai linahitaji elimu hata watoto wa kike hawata olewa katika umri mdogo kutokana na serikali kupeleka elimu kila sehemu.

Mkuu wa Chuo cha VETA Arusha Bagantabona Deusdedit Mrefu amesema kuwa Chuo cha VETA Arusha ndio kimejenga Chuo cha VETA Longido na samani za chuo hicho zimetengenezwa na wao wenyewe kwa kushirikiana na walimu pamoja wanafunzi.

Amesema kuwa ujenzi huo ulikuwa wa Mfumo wa Force Account ambapo walishirikisha mafundi wazawa na huduma zingine zote za ujenzi walizitoa kwa wananchi wa wilaya ya Longido na kuongeza kuwa wanashukuru wananchi kwa ushirikiano walionesha katika hatua za awali hadi kukamilika kwa Chuo hicho.

Amesema kuwa wanatarajia kuanza kutoa kozi fupi ambazo ni Ushonaji ,Uhazili , Ujenzi ,Udereva pamoja na umeme na baadae wataanza na kozi pale watapoweka mitambo mbalimbali ya kufundishia.

Kwa upande wa Mwalimu wa Usimamizi wa Ujenzi George Mosha amesema kuwa katika ujenzi huo umekuwa na ushirikishwaji kwa wananchi katika kushiriki ujenzi huo na hatimae kukamilika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad