NDOMBA:KIBAHA KUJENGA HOTELI YA KISASA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 22, 2023

NDOMBA:KIBAHA KUJENGA HOTELI YA KISASA

 Na Khadija Kalili, Kibaha

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Mji Kibaha Musa Ndomba amesemakuwa Madiwani wa Kibaha Mjini pamoja na Halmashauri hiyo wamejipanga kujenga Hoteli yenye hadhi ya kisasa ambayo itasheheni huduma zote muhimu na zenye hadhi ya nyota tano itakayojengwa mkabala na Njuweni kwani wa miliki ardhi yenye ukubwa.

Mheshimiwa Ndomba amesema hayo leo asubuhi kwenye kikao cha wazi cha Baraza la Madiwani kilichoketi kwa minajili ta kupitisha Bajeti ya 2023 -24.

"Ujenzi wa Hoteli hii una lengo la kuongeza vyanzo vya mapato kwa Halmashauri na kuimarisha nguvu ya fedha kwa kuanzisha miradi mingine mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujenga shule za msingi na sekondari sanjari na Zahanati katika Kata ya Tangini, Mkuza ambako hivi sasa wananchi wanakabiliwa na changamoto ya kukosa huduma hizo muhimu katika jamii" amesema Ndomba.

Kikao hicho kimefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mkoani Pwani.

"Tumepanga hoteli itajengwa ukwa awamu ambapo utaanza kwa kiasi cha Milioni 500 ,aidha amemuomba Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassan kuipandisha hadhi Halmashauri ya Kibaha na kuwa Manisapaa kwa sababu imekidhi vigezo vyote kwani Mkoa wa Pwani umeanzishwa mwaka 1975" amesema Ndomba.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Selina William amesema kuwa katika bajeti ijayo watakua wakali zaidi kwa kuhakikisha wanafuatilia fedha inayotoka na kuhakikisha miradi yote inakamilika kwani mradi unapochelewa wanaopata taabu ni wananchi katika eneo husika.

Diwani Viti Maalumu Chama Cha Mapinduzi Visiga Doris Paul amesema kuwa anatoa pongezi kwa uongozi kwa mpango wa kujenga Hoteli ya kisasa Kibaha kwa sababu hapa ndiyo lango la Jiji la Kibiashara Dar es Salaam pia ni Halmashauri yenye sifa ya kuwa na uwekezaji wa viwanda vingi nchini pia kuna fursa za uwekezaji hivyo ujenzi wa hoteli hii utakidhi mahitaji ya malazi kwa wawekezaji na wafanya biashara kwa ujumla ikiwemo kukuza uchumi na kipato cha wakaazi kwa ujumla.

Katika kikao hicho Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Kibaha Protas Dibogo aliwasilisha mapendekezo ya bajeti mwaka wa fedha 2023/2024 ili wajumbe wa Baraza waweze kupitia na kupitisha kiasi cha Sh.Mil 48,655,452,256.03 ikiwa ni vyanzo vya ndani,ruzuku kutoka serikali kuu, mchango wa jamii na kutoka kwa wafadhili wengine kwa ajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo,kulipa mishahara ya watumishi na kuendesha shughuli za ofisi kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Kutoka Kushoto ni Mwenyekiti wa  Halmashauri ya Mji Kibaha Mussa Ndomba akiwa na Makamu Mwenyekiti  Celina William (Diwani Viti Maalumu Chama Cha Mapinduzi).
Wa kwanza Kushoto ni Diwani wa Viti Maalum  Visiga  Doris  Paul akiwa na Madiwani  wenzake wakifuatilia mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad