HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 23, 2023

BONDIA SELEMANI KIDUNDA AACHA SINTOFAHAMU KUTOKUFIKA KUPIMA UZITO KWA AJILI YA PAMBANO LA KESHO

 Na Khadija Seif, Michuzi TV

BONDIA Selemani Kidunda ameacha sitofahamu kwa Mpinzani wake Raia wa (DRC)Patric Mukala baada ya kutojitokeza kupima uzito ikiwa ni maandalizi ya siku moja ya Pambano la ngumi za kulipwa linalotarajiwa kufanyika Februari 24,2023 Ukumbi wa Ubungo plaza Jijini Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya kupima uzito Mabondia , Mkurugenzi wa Kampuni Kemmon Agency ambaye pia ni Promota wa Pambano hilo Sada Salim amesema amesikitishwa sana na kitendo alichofanya Selemani Kidunda kwani walishasainiana Mkataba hivyo Pambano lipo palepale na asipotokea atatakiwa kulipa fedha alizopewa na fidia kutokana na kukiuka Mkataba wa makubaliano yao.

Sitofahamu hii imekuja baada mzani wa Kidunda kupanda jukwaani na kupima uzito lakini baada ya mshereheshaji wa zoezi hilo kupitia siyo yeye wala wapambe wake hali iliyomlazimu kwa muda Mpinzani kupima uzito mwenyewe na kutofanya (Face off) mpaka anaondoka uwanjani Kidunda hakutokea

"Selemani Kidunda acha Woga njoo uwanjani uonyeshe Umwamba wako ulingoni usiogope kupigwa hata Thaison alivuma sana kushinda kila Pambano lakini aliwahi kupigwa acha janja janja tunataka tuone vitasa "amesema Promota Sada

Katibu wa kaminsheni wa ngumi za Kulipwa nchini (TPBRC)Yahya Poli amesema mpaka leo hawana taarifa yeyote ya Selemani Kidunda kufika hivyo kulingana na sheria ya ngumi za kulipwa hivyo ajitokeze kupima uzito mbele ya Mpinzani wake na aingie kwenye Pambano hilo hapo kesho

"Itakapofika saa nane na nusu Mchana kama Selemani Kidunda hajatokea kupima uzito au kutoa taarifa zenye mashiko Pambano lake litafutwa ambalo kimsingi ndiyo kuu hivyo atachukuliwa sheria kali ikiwemo kulipa gharama au fidia "amesemaYahya.

Aidha wito umetolewa Kwa wanaopenda burudani hiyo kununua tiketi za kuingia katika Ukumbi wa Ubungo Plaza kutazama mubashara Mpambano huo kupitia Azam Media ni kuwani Mkanda wa ABU Uzito wa Super Middle.
Bondia Patric Mukala Raia wa (DRC) akipima Uzito Kwa Kwa ajili ya pambano la kesho dhidi ya Mpinzani Bondia wa JWTZ Selemani Kidunda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad