HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 21, 2023

ASASI ZA USIMAMIZI WA TAKA ZAHIMIZA WAOKOTA TAKA KUTAMBULIWA NA KUTHAMINIWA

 Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

TUKIWA tunakaribia kuadhimisha Siku ya Waokota Taka Duniani mnamo Machi 1, 2023, taasisi za Nipe Fagio na Takaniajira Foundation wametoa wito kwa serikali na asasi za kiraia kutambua na kuthamini jitihada za Waokota Taka katika kuyafanya mazingira ya nchi kuwa safi na salama kiafya.

Taasisi hizo mbili zimeungana mikono kuandaa mfululizo wa matukio, ikiwa ni pamoja na usajili wa Waokota Taka,Siku za Huduma kwa Jamii na Mkutano wa kitaifa mnamo tarehe 9 Machi kama sehemu ya ‘Programu ya Waokota Taka' ambao unalenga kutambua umuhimu wa Waokota Taka na mchango wao katika sekta ya usimamizi wa taka.

Siku za Huduma kwa Jamii zinafanyika kutoka Februari 10 hadi Februari 16 jijini Dar es salaam kama njia ya kuwapa motisha Waokota Taka na kusheherekea nao kwa kuwapa huduma muhimu kama uchunguzi wa kimatibabu kujua hali yao ya kiafya, milo na vinywaji, huduma za ususi na unyoaji nywele, nk.

Akizungumza wakati wa tukio hilo huko Mji Mwema katika manispaa ya Kigamboni, Kkurugenzi Mtendaji wa Nipe Fagio, Ana Le Rocha alisema: "Tunafurahi kurudisha fadhira kwa Waokota Taka kwa njia hii maalum na yenye maana ya kuheshimu mchango wao katika sekta ya urejelezaji taka na mazingira kwa ujumla.

Ndiyo sisi pamoja na Taka Ni Ajira, tunahimiza serikali na jamii nzima kuheshimu kazi zao kwa kutambua na kuthamini mchango wao,"Ana alisema.

Ana alisema kuwa ingawa mchango wa Waokota Taka katika sekta ya usimamizi wa taka ni muhimu, waokota taka wanakabiliwa na changamoto nyingi na viatarishi vingi katika maisha yao. "Wako katika mazingira magumu kwani wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na viatarishi vya kiafya, kwa hivyo tunatumai kuwa huduma kama hizi zinazotolewa wakati wa Siku za Huduma kwa Jamii zitakuwa muhimu kwao," alibainisha.

Kwa upande wake, Afisa wa Uhamasishaji wa Jamii wa Nipe Fagio, wakati akielezea mfululizo wa matukio yaliyofanywa hadi sasa tokea wiki iliyopita, Bw. Amiri Bakari alisema: "hadi sasa zaidi ya waokota taka 400 kutoka Jangwani (Ilala), Kibo (Ubungo), Saku (Temeke ), na Feri (Kigamboni) wamepata huduma mbali mbali za jamii, haswa uchunguzi wa kiafya na leo tumesajili waokota taka wengine zaidi ya 405 hapa Dampo la Pugu, Ilala."

Alifafanua pia kuwa mbali na Siku za Huduma kwa Jamii, Nipe Fagio pamoja na Taka Ni Ajira Foundation wanaandaa 'Mkutano Mkuu wa Waokota Taka' ambao utawaleta pamoja waokota taka, wafanyikazi katika sekta ya taka wasio rasmi, wadau wa usimamizi wa taka, na vyombo vya habari katika eneo moja ili kushea siri ya mafanikio yao, changamoto, na kuchangia upatikanaji wa kutambuliwa kwa waokotoka wa muda mrefu wa watendaji hawa muhimu katika sekta ya usimamizi wa taka.
Mmoja wa waokota taka akipatiwa huduma ya kitabibu na Dkt Emmanuel John (Kushoto) kutoka katika kituo cha afya Magrefa Healthcare Clinic katika Siku ya Huduma kwa Waokota Taka iliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Nipe Fagio na Taka Ni Ajira Foundation iliyofanyika katika maeneo ya Dampo la Pugu, manispaa ya Ilala, Ijumaa jijini Dar es Salaam. Zaidi ya Waokota Taka 400 walipatiwa huduma za kiafya, chakula, na burudani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad