HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 20, 2023

WAZIRI MBARAWA KUSHUHUDIA WADAU WA SEKTA YA USAFIRISHAJI WAKIKAA MEZA MOJA KUTATUA CHANGAMOTO ZAO KESHO JIJINI DAR


Na Mwandishi Wetu

WANACHAMA zaidi ya 250 wa Chama Cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) wanatarajia kushiriki kwenye mkutano Mkuu wa Chama hicho utakaofanyika hapo kesho Jumamosi jijini Dar es Salaam, ambapo Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa atakuwa mgeni rasmi.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaamu,Mwenyekiti wa TATOA amesema kuwa mkutano wao wa Saba wa mwaka utafanyika katika Hoteli ya Johari Rotana na madhumuni ya mkutano huo ni kuwaleta wasafirishaji wote wa sekta ya uchukuzi pamoja ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na sekta ya usafirshaji.

"Hii inajumuisha changamoto zote zinazoikabili
sekta ya usafirishaji. Mkutano huo utajumuisha wadhamini ambao watakuwa wakiwasilisha,kuonesha bidhaa na huduma zao ambazo zinaongeza utendaji kazi katika sekta ya usafirishaji..

"Wadhamini hao kwa pamoja ni Total Energies, benki ya NBC, Double Click, UTrack, GF trucks & equipment na korridor. TATOA ni chama cha hiari cha wafanya biashara yakusafirisha mizigo kwa njia ya barabara ndani na nje ya Tanzania, hususani katika nchi zilizo katika kanda ya jumuiya ya kusini wa Afrika (SADC).

"Na jumuiya ya AfrikaMashariki (EAC).DRC (Katanga, Mikoa ya Kivu ya Kaskazini na Kusini), Zambia, Malawi,Zimbabwe, Rwanda, Burundi, Uganda, naSudan Kusini. Ilianzishwa mwaka 2005 ikiwa na wanachama 25 pekee.TATOA imekua na kuwa chama cha wafanyabiashara waliojitolea ambao wanaona sekta ndogo ya usafirishaji wa barabara inakuwa mchangiaji namba 2 wa Pato la Taifa kuwa na wanachama zaidi ya 900," alisema Lukumay .

Aidha Lukumay alifafanua kuwa Mkutano Mkuu wa 7 wa Mwaka wa TATOA unatarajia kuhudhuriwa zaidi ya Wanachama 250 ambao ni wamiliki wa kampuniza usafirishaji . Wafadhili kutoka Totalengies, Benki ya NBC, Doubleclick-U-track, GFtrucks and equipment, korridor watatoa suluhisho ya mambo mbali mbali yanayohusiana na sekta , hiyo ni kupitia maonesho ya bidhaa pamoja na huduma wanazotoa.

Kwa upande wake Meneja Masoko na Mawasiliano wa GF Trucks and Equipment, Smart Deus, aliwahimiza wanachama wa chama hicho kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo huku akieleza kuwa wana ofa mbalimbali kwa ajili ya wateja wao.
"Katika mkutano huo tutatangaza kampeni maalum ya kutoa huduma za kiufundi bila malipo kwa malori yanayopita katika Barabara kuu ya Morogoro kwenda nchi jirani," Alisema Deus.

Katika hatua nyingine Meneja wa kitengo cha vilainishi kutoka Total Energies, Ally Saleh amesema kampuni hiyo imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na TATO.
"Kwetu sisi wasafirishaji ni wengi kuliko wateja kwa sababu licha ya kununua mafuta na mafuta kutoka kwetu tunawafuatilia ili kuhakikisha vifaa vyao vinafanya kazi ipasavyo na kwa ufanisi," alisema Salehe

Mgeni rasmi katika mkutano huo atakuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof Makame Mbarawa na wakuu wa mashirika mbalimbali ya serikali ikiwemo,TPA, TRA, LATRA, EWURA, TANROADS, GCLA, TASAC. Wanachama pia watapata fursa ya kuunganishwana wanachama wengine kutoka katika sekta hiyo
ya usafirishaji.
Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA), Elias Lukumay akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mkutano mkuu wa mwaka kujadili changamoto zao mbalimbali utakaofanyika jijini Dar es Salaama kesho Jumamosi.

Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA), Elias Lukumay akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mkutano mkuu wa mwaka kujadili changamoto utakaofanyika jijini Dar es Salaama kesho.Kulia ni Meneja masoko na mawasiliano wa kampuni ya GF Trucks & Equipments Ltd Smart Deusi na katikati ni Mkurugenzi mwendeshaji wa kampuni ya Double luck consulting ltd, Sandeep Basra na kushoto ni Meneja wa kampuni ya Total Energies, Ally Saleh

Meneja Masoko na Mawasiliano wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd, Smart Deusi akizungumza na wandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mkutano mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) kujadili changamoto mbalimbali utakaofanyika jijini Dar es sdalaam kesho, Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA), Elias Lukumay na katikati ni Mkurugenzi mwendeshaji wa kampuni ya Double luck consulting ltd, Sandeep Basra.

Meneja wa kampuni ya Total Energies, Ally Saleh akizungumza na wandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mkutano mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) kujadili changamoto mbali mbali utakaofanyika jijini Dar es sdalaam kesho.Wengine ni Mwenyekiti wa Chama hicho, Elias Lukumay , Mkurugenzi mwendeshaji wa kampuni ya Double luck consulting ltd, Sandeep Basra na kulia ni Meneja masoko na mawasiliano wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd Smart Deusi .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad