WADAU WA ELIMU WAASWA KUDUMISHA WELEDI ILI KUINUA KIWANGO CHA ELIMU - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 11, 2023

WADAU WA ELIMU WAASWA KUDUMISHA WELEDI ILI KUINUA KIWANGO CHA ELIMU

Sehemu ya Maafisa Elimu Kata mkoa wa Kigoma waliohudhuria na kushuhudia utiaji saini wa Mikataba ya utendaji kazi kati ya Afisa Elimu Mkoa na Maafisa Elimu Wilaya za Mkoa wa Kigoma
Afisa Elimu Mkoa wa Kigoma akimkabidhi Mkataba wa utendaji kazi Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Kobondo Julius Katyama
Afisa Elimu Mkoa wa Kigoma Pauline Ndigeza akimlabidhi Mkataba wa Utendaji kazi Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Kigoma Exavery Ntambala
 
Na. Andrew Mlama-Kigoma

Wadau wa Elimu mkoani Kigoma wametakiwa kuzibadili changamoto kuwa fursa kwa kutanguliza uzalendo na kudumisha weledi katika kutekeleza mikakati mbalimbali inayoandaliwa na Serikali ili kuboresha na kuinua kiwango cha Elimu.

Wito huo umetolewa na Kaimu Katibu Tawala Msaidizi upande wa Elimu Mkoa wa Kigoma Paulina Ndigeza, alipokuwa anafungua Kikao kazi cha Utiaji Saini Mkataba wa Utendaji Kazi baina yake na Maafisa hao kilichofanyika wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.

Ndigeza amesema kuwa dhamira ya Serikali kupitia mkataba huo ni kuhakikisha yanafanyika maboresho makubwa katika Sekta ya Elimu ili kuimarisha hali ya utendaji kazi katika mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji ili kuinua kiwango cha Elimu sambamba na ufaulu nchini.

Serikali inawekeza kiasi kikubwa cha Fedha katika kukabili changamoto na kuboresha miundombinu ya Elimu nchini. Hivyo watendaji wameshauriwa kufanya kazi kwa weledi ili kurejesha thamani ya Fedha ambayo Serikali inaendelea kuwekeza katika Sekta ya Elimu.

Aidha Ndigeza amesisitiza Maafisa Elimu Sekondari kwenda kusimamia vigezo vyote 22 vya upimaji wa utendaji kazi vilivyoainishwa kwenye mikataba waliyoisaini ili kuleta matokeo chanya kwa kuongeza ufaulu katika matokeo ya mitihani ya kuhitimu  Darasa la Saba, Kidato cha Nne na Sita.

Naye Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Kibondo Julius Kakiama, amesema vigezo vilivyomo kwenye mikataba hiyo vitawaongezea ari  ya utendaji kazi kwani inatoa fursa ya kila mtendaji kujipima na kujitathimini kisha kujua mapungufu yake na hatua za kuchukua ili kutimiza malengo yaliyowekwa.

‘‘Unapokuwa na mwongozo kama huu uliomo kwenye mkataba unarahisisha  kufahamu majukumu unayopaswa kuyatekeleza na kutambua hatua uliyofikia kiutekelezaji hivyo kuruhusu uwezekano mkubwa wa kupata matokeo chanya’’ amesema Julius.

Upande wake Afisa Elimu Kata Ruben Kahuza amesema kupitia kikao hicho wamejifunza namna ya kuzibadili changamoto kuwa Fursa ili kuepuka sababu zozote zitakazosababisha kushindwa kutekelezwa kwa vigezo vya upimaji vilivyomo kwenye mkataba wa utekelezaji.

Pamoja na uwepo wa changamoto ya kutotosheleza kwa ikama ya walimu, umbali kutoka makazi hadi shule zilipo pamoja na uelewa duni wa baadhi ya wazazi kuhusu ushiriki wa masuala mbalimbali ya kielimu. Watendaji tunapaswa kuzibadili na kuzifanya fursa ili kuhakikisha malengo yaliyowekwa na Serikali ili kuinua ufaulu yanafikiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad