Baada
ya kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha nne na Baraza la mitihani la
Tanzania (NECTA), Shule ya sekondari ya Feza Boys imefanikiwa kuongoza
kwa ufaulu wa juu ambapo wanafunzi wote 69 wamefanikiwa kupata division
one, kati ya hao, wanafunzi 44 wamepata division 1.7 huku wanafunzi 15
katika masomo yote wamepata alama A.
Hii ni kutokana na juhudi za
serikali ya awamu ya sita kupitia wizara ya elimu, kuweka mazingira
mazuri na wezeshi hasa katika kutoa ushirikiano mashuleni kuhakikisha
wanafunzi wanapata elimu bora.
Akizungumza na waandishi wa habari
le jijini Dar es Salaam, Mwalimu wa Taluma wa shule ya Feza Boys
Richard Mahina, amesema wanafunzi hao walipokua kidato cha pili
walifanikiwa kuingia kwenye 10 bora katika mtihani wa Taifa mwaka 2020
ambapo wameendeleza ubora wao mpaka kufikia kidato cha nne.
"Ufaulu
huu ni mzuri sana, ni fahari kubwa sana kwetu kama walimu,kama nchi
yetu na jamii kwa ujumla kwasababu kikubwa unachotakiwa kwa mwalimu ni
ufundishe na utoe matunda yaliyobora "
Pia kutokana na Baraza la
mitihani la Tanzania, NECTA kusitisha utaratibu wa kutangaza shule 10
bora na wanafunzi bora kwa matokeo ya kidato cha nne kwa sababu
iliyoelezwa kwamba ni utaratibu usio na tija, Mhina amesema wameupokea
vizuri uamuzi huo na wapo pamoja na serikali.
"Ni kweli wanafunzi
wanasoma katika mazingira tofauti, kikubwa ni kwamba wanafunzi wanasoma
vizuri na bahati nzuri wanafunzi wetu wamefanya vizuri sana hivyo tupo
pamoja na serikali uamuzi waliouchukua ni mzuri na sisi tunauunga mkono "
Maina
amewapongeza wanafunzi wote wa kidato cha nne wote 69 ambao
wamejitahidi kwa kuhakikisha wanakuwa na uthubutu katika masomo yao na
kupeleka kutoa matokeo mazuri shuleni hapo.
Aidha Maina
amewashukuru wazazi wa wanafunzi hao lakini pia uongozi wa feza schools
kwa kuwapa ushirikiano hadi kupelekea kupata matokeo hayo huku akiwataka
walimu wengine kuchukua mfano huo wa walimu wa mwaka jana.
Kwa
upande wake Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule ya Feza Boys, Bussury Omary
amesema walitarajia wanafunzi wao wangefanya vizuri kutokana na juhudi
walizokuwa nazo katika kutaka kujifunza na kuwa na uelewa wa kutosha.
"Walituaminisha
kwamba wanaweza na kweli wamefanikiwa, tunawashukuru wazazi, uongozi,
walimu na wanafunzi wenyewe kwani wanafunzi hawa walichokifanya
kinahitaji heshima ya juu, pia tunaishukuru serikali kwa kuondoa
utaratibu wa kutaja shule na mwanafunzi bora kwani inaweza ikasaidia
sana kuondoa wizi kwenye mitihani "
Omary amesema wanafunzi wote
ambao wamefaulu wanawapatia zawadi kutokana na ufaulu wake lakini pia
walimu ambao wamefanya wanafunzi hao kupata ufalu huo wanapewa pongezi
zao.
Naye Mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya Feza Boys
aliwapongeza wanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2022 kwa ufaulu wao
mzuri, hali inayowapelekea wao kupata morari ya kusoma zaidi na hata
kufanya vizuri zaidi katika mitihani yao ya mwaka huu.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Feza boys wakishangilia baada yabkutangazwa kwa matokeo ya kidato cha nne na shule hiyo kuongoza kwa kufaulisha division one kwa wanafunzi woote waliomaliza shuleni hapo
No comments:
Post a Comment