HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 13, 2022

WIZARA YA ELIMU YAZUNGUMZIA UMUHIMU UCHANGIAJI CHAKULA SHULENI, WFP, WADAU WAUJADILI MUONGOZO

 

 
Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Morogoro

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesisitiza umuhimu wa kuendelea kutoa elimu zaidi kwa jamii ili kutambua malengo ya kuchangia gharama za chakula shuleni.

Mratibu wa Masuala ya Lishe Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Grace Shileringo ameeleza hayo leo Desemba 13 mwaka 2020 Mjini Morogoro wakati akizungumza waandishi wa habari katika uzinduzi wa muongozo wa utekelezaji wa sera ya mpango wa chakula shuleni sambamba na kuanzisha timu ya wataalamu itakayokuwa ikifuatilia utekelezaji wa mchakato huo.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi na mashirika binafsi likiwemo la Mpango wa Chakula Duniani (WFP).

Amesema jamii imekuwa na dhana potofu ya kutochangia gharama za chakula mashuleni kwa sababu ya kuwepo kwa sera ya elimu bure hivyo amesisitiza suala la chakula ni jukumu la wazazi na walezi na halina uhusiano na sera ya elimu bure.


"Niwaombe wazazi na jamii kwa ujumla, utekelezaji wa mpango huu wa chakula mashuleni ni jukumu letu kama wazazi, ni jambo lilosainiwa na Rais wetu na sisi tunafanya utekelezaji," amesema Shileringo.

Ameongeza kikao cha jana kimewakutanisha wadau mbalimbali zikiwemo Wizara za Kisekta kutoka Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na Shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa chakula Duniani (WFP), ambao wametoa msaada mkubwa kuhakikisha kikao hicho kinafanyika pamoja na utekelezaji wa maadhimio yake.

"Tunawashukuru wenzetu wa WFP ambao wamekuwa mstari wa mbele kutekeleza maadhimio ya Serikali kwenye masuala kama haya, lishe bora ni eneo ambalo wenzetu wa WFP wameweka mkazo,:" alisema Shileringo.Kwa upande wake akizungumza kwa niaba ya WFP, Mkuu wa idara ya lishe wa Shirika hilo, Vera Kwara, alisema WFP imekuwa ikisaidia masuala ya chakula shuleni kwa miaka mingi.

Amefafanua Serikali ya Tanzania imefanya jambo jema kukubali na kuzindua mpango huo wa chakula mashuleni utakaosaidia ustawi wa jamii na ufaulu pia wa wanafunzi mashuleni.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Idara ya elimu Maandalizi na Msingi wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar, Fatuma Mode Ramadhani, amesema suala la chakula mashueni Zanzibar wameanza kulitekeleza muda mrefu lakini mkazo ulikuwa kwa wanafunzi wa shule za awali.

"Kwa sasa tumeanza kwa shule za msingi, tumekuja hapa kujifunza namna wenzetu wanavyotekeleza mpango huu, sis tayari tumeanza na shule zilizopo maeneo ya vijini na mpaka sasa kuna shuke 37 zinazotekeleza mpago huu vijijini," amesema.

Kwa upande wake Ofisa Lishe kutoka ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Neema Kweba, alisema mpango huo wa chakula mashuleni unasimamiwa kuanzia ngazi ya mkoa mpaka ya Kata.

"Tumetengenezewa mpango wa utekelezaji wa muongozo ambao unaenda kukamilika hivi karibuni, lengo ni kuhakikisha huduma ya chakula na lishe mashuleni inatekelezwa na kama tunakumbuka Septemba 30 mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan alisaini mkataba na wakuu wa mikoa kwa ajili ya utekelezaji wa sera hii," amesema Kweba.

Mkuu wa Idara ya Lishe wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Vera Kwara akielezea namna ambavyo shirika hilo katika kusaidia Mpango wa Chakula shuleni ambapo ametumia nafasi hiyo kusisitiza wataendelea kusaidiana katika kufanikisha Mpango huo.
Wadau wa masuala ya lishe nchini wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufunguliwa kwa kikao kazi cha siku mbili kinachofanyika mkoani Morogoro.Kikao Cha wadau hao pamoja na mambo megine wataweka mkakati wa kutekeleza Sera ya Chakula shuleni sambamba na kuunda timu ya watalaamu watakaofanikisha kutekelezwa kwa mpango huo.
Mratibu wa masuala ya Lishe kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Grace Shileringo akizungumza mbele ya wadau wa Lishe leo Mjini Morogoro wakati wa Kikao kazi kujadili utekelezaji wa mpango wa cakula shuleni.
Mratibu wa masuala ya Lishe kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Grace Shileringo  akitoa madambele ya wadau wa Lishe leo Mjini Morogoro wakati wa Kikao kazi hicho
Msimamizi wa Elimu kutoka World Vision Tanzania Jennifer Mhando akiandika notisi muhimu wakati wa Kikao hicho
Mkurugenzi Idara ya Elimu Maandalizi na Msingi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibari Fatma Mode Ramadhan akifafanua jambo kuhusu Mpango wa chakula shuleni wakati wa Kikao kazi Cha wadau wa Lishe kinachofanyika Mjini Dodoma
Ofisa Lishe kutoka Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) Idara ya Afya , Ustawi wa Jamii na Lishe Neema Kweba akizungumza wakati wa kikao hicho
Mratibu wa masuala ya Lishe kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Grace Shileringo (kushoto) akiwa na Mkuu wa Idara ya  Lishe kutoka Shirika la Mpango wa chakula Duniani (WFP) Vera Kwera (kulia) wakifuatilia kwa umakini majadiliano ya wadau wa lishe nchini






Matukio ya katika Wakati wa kikoa kazi cha wadau wa Lishe wakijadiliana namna ya kutekeleza Mpango wa Chakula shuleni.( Picha zote na Said Mwishehe -Michuzi Blog)
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad