Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
KAMPUNI
ya Gama Gaming Limited imezindua jukwaa lake la kwanza la Mchezo wa SMS
liitwalo BAHATI, ambalo litatoa uzoefu mzuri wa michezo ya kubahatisha
ili kukidhi haja ya Watanzania kwa michezo mbalimbali ya kucheza kwenye
USSD kupitia Mobile Money Wallets na baadaye kwenye majukwaa mengine.
Akizungumza leo Desemba 13,2022 jijini Dar es Salaam , Mkuu wa Masoko na Mawasiliano Gama Gaming Limited Asungushe Mtetemela amesema wataanza na Mtandao wa Simu za Mkononi Vodacom na Tigo na baadaye kuongeza Airtel na Halotel kama washirika wakati mchezo ukiendelea na kukua.
Amesema nia yao ya kuingia sokoni ilikuwa kuleta michezo na burudani mbalimbali ambazo zilihitajika sana." Hatuwezi kusubiri kuwaonyesha watazamaji na wachezaji wetu kile tunachowawekea katika uuzaji wetu, michezo yetu, shughuli zetu za kijamii na burudani tuliyo nayo.
"Mchezo utakuwa na droo 3 katika saizi na viwango tofauti kulingana na mtu/mchezaji, ambazo ni; Dhahabu Sh.1,000, Almasi 2,000 na Tanzanite Sh.5,000 kwa kila mchezo au tiketi.Kila tiketi ya kucheza ina nafasi kadhaa za kushinda mwanzoni kila tiketi ina nafasi 2 za kushinda wakati wa jackpot ya papo hapo na jackpot ya kila wiki, jackpot zingine zitaongezwa kadiri mchezo unavyoendelea na kuongeza nafasi zaidi kwa kila uchezaji wa tiketi,"amesema.
Amefafanua kila droo ina uwezekano mkubwa wa kushinda na bei zinazovutia. Zawadi za dhahabu ni kati ya Sh 2,000 hadi 200,000, Almasi 5,000 hadi 500,000 na Tanzanite kutoka 10,000 hadi 1,000,000 kwa zawadi za papo hapo.
Ameongeza kuwa zawadi ya kila wiki ya jackpot itatangazwa kila wiki na washindi kutangazwa wakati wa onyesho la jackpot litakalofanyika kila wiki.Kama sehemu ya dhamira yao ya kuwashirikisha wateja wetu, bado hatujatoa programu nyingine zilizopo katika Bahati na namna ya kujiunga ikiwa ni pamoja na tovuti na utumiaji program kwa wiki zijazo, ambapo hii itarahisisha kuelewa kwa watumiaji wake.
Hata hivyo, kwa kuzingatia umri, sheria na kanuni zilizowekwa za michezo ya kubahatisha, tungependa kuendeleza uchezaji unaowajibika katika mfumo wetu wote. Kwa mtumiaji yeyote atakayetumia vibaya au kwenda kinyume na sheria na kanuni zilizowekwa atapigwa marufuku kushiriki katika bahati nasibu yoyote ya mchezo wa BAHATI ulio chini ya Gama Gaming.
"Kama sehemu ya wajibu wetu wa Kijamii tumepanga kuwa mwanachama hai katika jamii yetu na tutashiriki katika nguzo tatu ambazo tumeweka mkazo katika marekebisho ya elimu, maendeleo ya jamii na huduma ya afya. Kila nguzo itafunguliwa na kuzinduliwa tunapoendelea.Wateja wetu ni sehemu ya maisha yetu pamoja na sisi na mipango iliyopangwa pia inalenga kuwa sehemu ya mipango yao,"amesema Mtetemela.
Awali wakati anaelezea uzinduzi huo Mtetemela amesema mazingira ya michezo ya kubahatisha nchini Tanzania yamebadilika kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita tangu kuanzishwa kwake mwaka 1930 kupitia mchezo wa pool betting juu ya ushindani wa Simba na Yanga hadi kudhibitiwa mwaka 1967 kupitia sheria ya pools na bahati nasibu.
Amesema mazingira yamebadilika huku teknolojia ikichukua sehemu ya ukuaji wake na maslahi ya wachezaji. Hata hivyo, bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania imekuwa muhimu na katika kuweka kanuni na sera kusaidia ukuaji wa sekta hii.
"Hivi karibuni iliripoti kuhusu ukuaji wa asilimia 6 ya mapato kutoka kwa mapato ya mwaka jana ya Bilioni 132.Gama Gaming Limited ni kampuni ya michezo ya kubahatisha ambayo hivi karibuni imepewa leseni na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania kuendesha bahati nasibu ya SMS chini ya leseni SL000000005."
Meneja kutoka Kitengo cha TEHAMA -Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Kabora Mboya akieleza kanuni a sheria mbalimbali katika kushiriki michezo ya kubahatisha,amoengeza kuwa kwa kuzingatia umri, sheria na kanuni zilizowekwa za michezo ya kubahatisha kila atakataka kushiriki ni lazima azifuate.Picha ya pamoja
Mkurugenzi wa KAMPUNI ya Gama Gaming Limited Wilffred Magotti ( kulia) akimuelekeza Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya atambulikae kwa jina la Kisanii G Nako hatua kwa hatua namna ya kushiriki Mchezo huo wa SMS uitwao BAHATI.
No comments:
Post a Comment