HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 6, 2022

TIRA, T-PESA WAZINDUA HUDUMA ZA BIMA, SOKO LA BIMA KUKUA

Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dk. Baghayo Saqware (kushoto) akimpongeza Mkurugenzi wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde mara baada ya kuzinduwa huduma ya Bima ya T-Pesa inayotolewa na Kampuni T-Pesa leo jijini Dar es Salaam. 

Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Dk. Baghayo Saqware (kushoto) akizinduwa huduma ya Bima ya T-Pesa inayotolewa na Kampuni ya T-PESA kwa kushirikiana na makampuni mbalimbali za bima nchini leo jijini Dar es Salaam. Kulia pamoja naye ni Mkurugenzi wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde.

Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima nchini Tanzania (TIRA), imeipongeza Kampuni Tanzu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) T-Pesa kwa kuanzisha huduma za bima mbalimbali ijulikanayo kama Bima ya T-Pesa kupitia mtandao wa simu za mkononi.

Pongezi hizo zimetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kamishna wa TIRA, Dkt. Baghayo Saqware alipokuwa akizinduwa rasmi huduma ya Bima ya T-Pesa inayotolewa na Kampuni ya T-PESA kwa kushirikiana na makampuni anuai ya bima nchini leo.

Alisema kwa hatua hiyo, T-Pesa inakuwa ni moja ya wadau watoaji wa elimu ya bima nchini, kwani itakuwa na kazi pia ya kusimamia uhai, uhimilivu na uendelevu wa soko la bima, ili kuchangia ukuaji wa sekta ya bima.

"...Nawapongeza kwa kuwa sehemu ya watoa elimu ya bima hapa nchini, tuna kazi ya kusimamia uhai, uhimilivu na uendelevu wa soko la bima, ili kuwezesha kukua kwa sekta ya bima. Lazima kuwe na mikakati, ya kusajili watoa huduma wa bima mbalimbali, ambao pia wanaweza kuwafikia wananchi wahitaji sehemu mbalimbali hapa nchini.

Aliongeza kuwa TIRA imevutiwa zaidi na huduma hizo za Bima ya T-Pesa kwani baadaye itawanufaisha pia wakulima, wafugaji pamoja na wavuvi licha ya kutoa huduma nyingine anuai za bima kwa jamii.

Wananchi wanaitaji elimu ya bima vizuri, hivyo ni matarajio ya Serikali T-Pesa pamoja na washirika wenu mtakwenda kutimiza azma yenu nzuri kwa kufuata weledi wenye kuzingatia sheria za bima za nchi.

Aidha Kamishna huyo alisema, Serikali inataka huduma za bima ziwe sehemu ya utatuzi wa matatizo ya jamii yetu, ikiwemo ni pamoja na kuondoa umaskini, na kuongeza utajiri kwa wananchi.

Awali akizungumza, Mkurugenzi wa T-PESA, Bi. Lulu Mkudde alisema T-Pesa kwa kuanzia itatoa huduma za bima ya Magari, Bima ya Nyumba, Bima za ajali. Akifafanua zaidi Bi. Mkudde alisema mteja atatakiwa kupiga *150*71# kisha namba 7-Huduma ya Bima na T-Pesa kisha kufuata maelekezo mengine.

"...Hakika T-Pesa imeleta urahisi kwa wateja wake kufanya manunuzi ya Bima moja kwa moja kutoka kwenye simu zao za mkononi. Hakuna tena kutumia vitabu au kadi za bima za plastiki. Wateja wa T-Pewa wataweza kupata Bima zao kwa urahisi sambamba na kila kitu wanachoitaji ikiwemo orodha ya manufaa kwa muhusika na fomu za madai kupitia simu zao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad