HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 6, 2022

TGNP YATOA MAFUNZO KWA MASHIRIKA YANAYOTETEA HAKI ZA WANAWAKE NA USAWA WA KIJINSIA

  Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umeandaa mafunzo ya kuimarisha uwezo wa ushawishi na uchechemuzi kwa mashirika yanayotetea haki za mwanamke na usawa wa kijinsia yaliyoanza leo Desemba 06 hadi 09, 2022 yakiwa na lengo la kuongeza uelewa wa dhana ya kijinsia, kuongeza ujuzi wa washiriki wa ushawishi na uchechemuzi wa masuala ya kijinsi, kutambua fursa zilizopo kwa ajili ya kuwezesha uchechemuzi ngazi ya Serikali pamoja na kuandaa mikakati na mipango kwa ajili ya kujega sauti na utendaji wa pamoja na katika ushawishi na uchechemuzi wa masuala ya kijinsia.


Akizungumza Mwezesha wa Mafunzo hayo Mary Nsemwa amesema washiriki wa mafunzo haya ni wadau mbalimbali kutoka Taasisi mbalimbali  zunazoshughulikia masuala kijinsia pamoja na haki za wanawake hivyo wamekutanishwa hapa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ili kuwaongezea uelewa kuhusu masuala ya kijinsia ili waweze kuongeza ushawishi zaidi kwenye jamii.

Amesema Suala la ukatili wa kijinsia linatokea kwasababu nyingi lakini ukiangalia nyuma ya hili ni kuwa ukatili wa kijinisa umebeba nguvu na mfumo duni kwasababu  anayefanya ukatili anajiona yeye ndo mwenye nguvu kuliko anayemfanyia ukatili mfano ukatili wa mwanaume kwa mwanamke hii ni kutokana na Mwanume kujiona yeye ana nguvu  na hata jamii pia inamuona ni mtu wa tofauti au mwanamke kwa mtoto kwasababu yeye anauwezo wa kufanya chochote kwa mtoto wake.

pia amesema wadau hawa wakijengewa uwezo na kujenga sauti ya pamoja ya kukemea masuala yote ya ukatili wa kijinsia watakwenda kujenga msingi mzuri hasa kutengeneza vuguvugu na nguvu zaidi kwenye suala la kupunguza ukatili wa kijinisia maana zikiachwa ziendelee zitakuja kuleta madhara makubwa baadae kwenye jamii na hasa zitamuumiza sana Mama na mtoto.

Naye mnufauka wa mafunzo Selina Lyapinda ameushukuru Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kuweza kuwapa mafunzo hayo kwani yatawaongezea uelewa kwenye masuala ya kijinsia na kupambana na masuala haya kwenye jamii ambayo yamekidhiri.

\
Mwezesha wa Mafunzo Mary Nsemwa akiwasilisha mada iliyokuwa inahusu dhana za Jinsia na maana yake katika muktadha wa sasa wakati wa mafunzo ya kuimarisha uwezo wa ushawishi na uchechemuzi kwa mashirika yanayotetea haki za mwanamke na usawa wa kijinsia yaliyoanza leo Desemba 06 hadi 09, 2022 yakiwa na lengo la kuongeza uelewa wa dhana ya kijinsia yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwezeshaji wa Mafunzo hayo Deo Temba akiwasilisha mada kuhusu kuongeza ujuzi wa washiriki wa ushawishi na uchechemuzi wa masuala ya kijinsi na kijinsia wa mafunzo ya kuimarisha uwezo wa ushawishi na uchechemuzi kwa mashirika yanayotetea haki za mwanamke na usawa wa kijinsia yaliyoanza leo Desemba 06 hadi 09, 2022 yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakichangia mada zinazohusu namna ya kuongeza kuongeza ujuzi wa washiriki wa ushawishi na uchechemuzi wa masuala ya kijinsi na namna ya kuongeza uelewa wa dhana ya kijinsia kwa mashirika yanayotetea haki za mwanamke na usawa wa kijinsia wakati wa mafunzo yalioandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) yaliyoanza leo Desemba 06 hadi 09, 2022.
Baadhi ya washiriki wakijadiliana kwenye makundi  ili kuongeza kuongeza ujuzi wa washiriki wa ushawishi na uchechemuzi wa masuala ya kijinsi na namna ya kuongeza uelewa wa dhana ya kijinsia kwa mashirika yanayotetea haki za mwanamke na usawa wa kijinsia wakati wa mafunzo yalioandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) yaliyoanza leo Desemba 06 hadi 09, 2022.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad