HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 28, 2022

PROF. OLE GABRIEL AHIMIZA MAAFISA TEHAMA KUBORESHA MATUMIZI YA TEHAMA MAHAKAMANI

 


Na Tiganya Vincent-Mahakama ya Tanzania - DODOMA

Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel amewataka Maafisa wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kuboresha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa ajili ya kuwezesha uharakishaji wa utekelezaji wa jukumu la utoaji haki kwa wananchi.

Prof.Ole Gabriel alisema hayo leo wakati akifungua mkutano wa Maafisa TEHAMA kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini unaofanyika katika ukumbi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) cha Dodoma.

“Mifumo ikikaa vizuri itasaidia kupunguza mapungufu yaliyojitokeza katika utendaji mwaka uliopita."Naomba mboreshe mifumo yenu tunahitaji kuona TEHAMA inapewa nafasi katika utendaji kazi za Mahakama wa kila siku,"alisema Prof. Ole Gabriel.

Aliwataka Maafisa TEHAMA kuhakikisha wanaimarisha matumizi ya TEHAMA ili kuongeza ufanisi na tija katika utoaji wa haki kwa wananchi wengi kwa gharama nafuu.

Prof Ole Gabriel alifafanua zaidi ya kuwa mkutano huo ni muhimu kwa ajili kubadilisha uzoefu wa baadhi ya mambo na kuongeza kuwa hiyo ni heshima ya kipekee kabisa kwa sababu Mahakama inakwenda kubadilika katika matumizi ya TEHAMA.

Alisema msukumo walio nao ni kuimarisha zaidi matumizi ya TEHAMA kwa ngazi zote za Mahakama ambapo hadi sasa asilimia 99 ya mashauri yanafunguliwa kwa njia ya mtandao ili kuwarahisishia wananchi upatikanaji wa huduma katika mazingira nafuu.

Aidha ,Prof. Ole Gabriel alisema zaidi ya asilimia 70 ya mashauri yanatoka kwenye Mahakama za Mwanzo na kusema kuwa ni vema wakaweka nguvu katika kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika Mahakama hizo ili wananchi wengi nao waweze kufikiwa na huduma hizo.

Wakati huo huo Mtendaji Mkuu huyo wa Mahakama ya Tanzania alisema hivi sasa wameanzisha huduma mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kutoa maoni yao na kuuliza maswali pale wanapoona hawakutendewa haki ili wapate ufafanuzi sahihi kwa kutumia mifumo mbalimbali.

Alitaja huduma zinazoendelea ni Kipindi cha Sema na Mahakama cha kila siku ya Jumanne kuanzia saa 12.30 jioni hadi saa 1.30 usiku kupitia Runinga ya ITV na kile cha Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) cha siku ya Alhamis kuanzia saa 12.00 jioini hadi saa 1.00 usiku.

Prof. Ole Gabriel aliongeza kuwa njia nyingine ambayo imeanzisha ni kutoa maoni au kuuliza maswali kupitia Kituo cha Taarifa cha Mahakama ya Tanzania (Call Center) kupitia nambari 0752500400 au kupitia namba ya bila malipo ya 0800750247.

“Pia tumefungua laini ya kushugulikia ndoa mirathi pekee.Mikakati iliyopo ni kuboresha miundombinu ya TEHAMA na matumizi ya Mahakama mtandao hivyo tunakwenda kuwekeza zaidi kwenye eneo hili,” alisisitiza

Prof. Ole Gabriel aliwataka wananchi kutumia mifumo mbalimbali iliyoanziswa na Mahakama ya Tanzania kupata majawabu ya maswali na kero zao mbalimbali badala kusafiri na kutumia fedha nyingi kwa jambo ambalo suluhu yake angeipata akiwa kwake.

Aliongeza kuwa hivi sasa Mahakama ya Tanzania ipo kwenye hatua za mwisho za majaribio ya matumizi ya mfumo wa akili bandia ambayo itakuwa ikitafsiri mambo mbalimbali na kuandika nakala za hukumu.

Prof. Ole Gabriel aliwataka Maafisa TEHAMA kubadilika na kufikiria nje ya boksi ili waweze kuendana na kasi ya utendaji wa Mahakama kupitia kiongozi wao ambaye ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Kurugenzi ya TEHAMA(DICT) Enock Kalege alisema Maafisa hao wanakutano ili kutathimini utekelezaji wao wa Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania na kuboresha maeneo ambayo hawakufikia malengo.

Alisema mkutano huo unajumuisha Maafisa TEHAMA 49 kutoka Mikoa yote ya Tanzania bara.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa hotuba ya ufunguzi leo wa Mkutano wa Maafisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini ambao unaofanyika katika ukumbi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) cha Dodoma.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya TEHAMA(DICT) Mahakama ya Tanzania Bw.Enock Kalege alitoa maelezo ya utanguzi leo kabla ya ufunguzi Mkutano wa Maafisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini ambao unaofanyika katika ukumbi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) cha Dodoma.
Baadhi ya Maafisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) wa Mahakama ya Tanzania kutoka Mikoa mbalimbali wakifuatilia hotuba ya ufunguzi leo ya Mkutano wao ambao unaofanyika katika ukumbi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) cha Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa meza kuu leo baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Maafisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini ambao unaofanyika katika ukumbi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) cha Dodoma. Wengine ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma Mhe.Silvia Lushasi(kushoto) na kulia ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya TEHAMA(DICT) Mahakama ya Tanzania Bw.Enock Kalege.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel(katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Maaafisa TEHAMA wanawake wa Mahakama ya Tanzania leo baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Maafisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini ambao unaofanyika katika ukumbi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) cha Dodoma. Wengine waliokaa ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma Mhe.Silvia Lushasi(kushoto) na kulia ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya TEHAMA(DICT) Mahakama ya Tanzania Bw.Enock Kalege.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel(katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Maaafisa TEHAMA kutoka Makao makuu ya Mahakama ya Tanzania leo baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Maafisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini ambao unaofanyika katika ukumbi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) cha Dodoma. Wengine waliokaa ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma Mhe.Silvia Lushasi(kushoto) na kulia ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya TEHAMA(DICT) Mahakama ya Tanzania Bw.Enock Kalege.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel(katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Maaafisa TEHAMA kutoka Mahakama Kuu Divisheni mbalimbali leo baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Maafisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini ambao unaofanyika katika ukumbi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) cha Dodoma. Wengine waliokaa ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma Mhe.Silvia Lushasi(kushoto) na kulia ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya TEHAMA(DICT) Mahakama ya Tanzania Bw.Enock Kalege. Picha na Tiganya Vincent-Mahakama ya Tanzania

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad