HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 30, 2022

PRISONS WAKUTANA NA KIPIGO WASICHOTEGEMEA

 

Mshambuliaji wa Simba SC, aliyesajiliwa kwenye dirisha dogo, Saido Ntibazonkiza akishangilia moja ya bao lake katika mchezo huo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, dhidi ya Tanzania Prisons SC, Ntibazonkiza alifunga mabao matatu (Hat Trick) sanjari na Nahodha wa hiyo, John Raphael Bocco wakati Simba SC ikiondoka na ushindi mnono wa mabao 7-1 dhidi ya Maafande hao wa Jeshi la Magereza.

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
NI kweli waliahidiwa kitita cha Tsh. Milioni 30/- endapo wangepata ushindi dhidi ya Simba SC! lakini kilichowakuta Maafande hao wa Jeshi la Magereza wala hawakutegema, baada ya kupokea kichapo cha mabao 7-1 dhidi ya Mnyama kwenye mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (NBC PL) uliopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Kipindi cha kwanza, Tanzania Prisons SC waliwadhibiti Simba SC na kwenda mapumziko kwa sare ya bao 1-1 ikiwa baada ya Simba SC kutangulia kwa bao la Mshambuliaji John Raphael Bocco kwenye dakika ya 12’ baada ya kuonganisha ‘pasi ya assist’ ya Saido Ntibazonkiza.

Mshambuliaji wa Tanzania Prisons SC, Jeremiah Juma Mgunda alisawazisha kwa bao hilo kwenye dakika ya 29’, baada ya kupiga mpira wa juu uliomshinda Golikipa wa Simba SC, Aishi Manula na kuwapita kirahisi, Mlinzi Joash Onyango na Kiungo Mzamiru Yassin.

Katika kipindi cha pili, Simba SC walichachamaa kwa kulishambulia lango la Tanzania Prisons, ambapo kwenye dakika ya 46’ Nahodha John Bocco aliandika bao la pili baada ya kupokea ‘assist’ ya Pape Ousmane Sakho. Dakika ya 60, Saido Ntibazonkiza alikandamiza Msumari wa tatu kwa Tanzania Prisons SC.

Nohadha John Bocco aliendeleza mvua ya mabao kwa kuandika bao la nne kwa Tanzania Prisons kwenye dakika ya 62 baada ya kupigwa pasi safi ya Mwamba wa Lusaka, Clatous Chama. Ntibazonkiza alifunga bao la tano kwa ‘shuti’ kali la lililomshinda Kipa wa Prisons, Hussein Abel, dakika ya 69’ huku Mlinzi Shomari Kapombe alifunga bao la mwisho na la saba dakika ya 87’.

Baada ya ushindi huo, Simba SC wakiwa nafasi ya pili na michezo 19 wamefikisha alama 44 kwenye msimamo wa Ligi hiyo huku Yanga SC wakiwa kileleni mwa msimamo wakiwa na alama zao 47 huku wakiwasubiri Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa mzunguko huo wa 19.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad