HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 22, 2022

NAMTUMBO WAKAMILISHA UJENZI WA MADARASA 17 YA KIDATO CHA KWANZA 2023

 


NA YEREMIAS NGERANGERA, NAMTUMBO

Mkurugenzi wa Halmashauri  ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma  Chiriku Hamis Chilumba alisema  amekamilisha ujenzi wa madarasa  17 kwa shule 11 zilizokuwa na upungufu wa vyumba vya kusomea katika Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo.

Chilumba  alitanguliza shukrani zake kwa Raisi wa Jamhuri  ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan  kwa kuipatia Halmashauri ya Namtumbo fedha kiasi  cha shilingi milioni 340 ili kuondoa changamoto ya  upungufu  wa vyumba vya madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka  2023.

Michael  Lyambilo Afisa elimu sekondari wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo  alizitaja shule za sekondari  zilizokamilisha ujenzi wa madarasa hayo kuwa ni shule ya sekondari Korido,Narwi,Nasuli /Suluti ,Luchili,Nahimba,Lisimonji na shule ya sekondari  Msindo.

Lyambilo alizitaja shule zingine za sekondari zilizokamilisha ujenzi  huo wa madarasa   kuwa ni shule ya sekondari Nanungu,Selous,Namabengo pamoja na shule ya sekondari  Magazini  ambapo kwa sasa zipo tayari  kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza pasipo kuwa na wasiwasi wa upungufu wa madarasa.

Afisa manunuzi  wa Halmashauri hiyo Willy Ndabila kwa upande wake alidai pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika kukamilisha ujenzi wa madarasa 17 ya shule za sekondari 11 katika Halmashauri hiyo alizitaja changamoto  alizokumbana nazo katika utekelezaji wa ujenzi kwa kutumia local fundi.

Ndabila alifafanua changamoto  ya mafundi  kuomba kazi ya ujenzi  kwa kiasi kidogo cha fedha  na wakishapata kazi  ya ujenzi  kwa kiwango alichokiomba na kubainika kuwa  fundi huyo aliyepitishwa  na kamati ya ujenzi  kuwa ameomba kwa kiwango cha chini anategemea sehemu kubwa ya uendeshaji  wa kazi  hiyo kutegemea malipo kutoka  Halmashauri licha ya mikataba kueleza bayana kuwa awe na uwezo kufanyakazi bila kutegemea malipo ya awali kutoka Halmashauri.

Lakini pia Ndabila alifafanua changamoto nyingine  ya manunuzi  ya bei ya soko katika jamii bado inawapa  wakati mgumu na kutoeleweka katika jamii ,kwa  madai kuwa wazabuni waliopewa zabuni kuhudumia vifaa vya viwandani  hulipwa  kwa cheki na hizo cheki zinakatwa kodi hali inayosababisha wakati  mwingine kutonunua kwa bei  ya soko kulingana na mazingira .

Hali hiyo kamati za ujenzi  ,manunuzi,na usimamizi  za vijiji  hawaelewi hilo na kuelekeza  lawama zao kwenye kitengo cha manunuzi  cha Halmashauri na kudai  watumishi  wa kitengo hicho kuingia lawamani mara kwa mara kwa hoja ya kununua  vifaa vya viwandani  bei  isiyo ya soko .

Hata hivyo Ndabila alisema  Halmashauri  inaendelea  kutoa elimu kwenye kamati za ujenzi,manunuzi na usimamizi  za vijiji ili ziweze  kuelewa hilo na kushirikishana katika manunuzi ya vifaa vya viwandani ili kuondoa sintofahamu zinazojitokeza .

Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo  ina jumla ya shule 33 za sekondari  ambapo kati ya shule hizo, 25 ni za serikali , na 8 zisizo za serikali na shule 17 kati ya hizo 25 zilikuwa na upungufu  wa madarasa  na sasa zimekamilisha ujenzi  wa madarasa kuondoa upungufu uliokuwepo.





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad