HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 5, 2022

MKURUGENZI MKUU WA RUWASA ATEMBELEA CHOMBO CHA KUTOA HUDUMA YA MAJI NGAZI YA JAMII, MBALALI

Mkurugenzi Mkuu wa Ruwasa Mhandisi Clement Kivegalo kulia,akizungumza na baadhi ya viongozi wa Chombo cha kutoa huduma ya maji ngazi ya jamii(CBWSO)ya kijiji cha Mwakaganga na Majengo Halmashauri ya wilaya Mbalali mkoani Mbeya,ambapo amewapongeza viongozi hao kwa kazi nzuri ya kuendesha mradi wa maji ambao umewezesha wananchi wa vijiji hivyo kuondokana na kero ya huduma ya maji safi na salama. Na Muhidin Amri, Mbalali

VYOMBO vya kutoa huduma ya maji ngazi ya jamii nchini,vimetakiwa kuhamasisha jamii kuunganisha huduma ya maji kwenye kaya zao ili kupata fedha za kujiendesha bila kutegemea ruzuku ya serikali.

Wito huo umetolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa Mhandisi Clement Kivegalo,mara baada ya kukagua chombo cha watoa huduma ya maji ngazi ya jamii(CBWSO)katika kijiji cha Majengo na Mwakaganga wilaya ya Mbalali mkoani Mbeya.

Mhandisi Kivegalo alisema,hatua hiyo itasaidia miradi mingi ya maji inayojengwa na serikali kuwa endelevu na kutoa huduma bora ya maji kwa wananchi katika maeneo mengi hapa nchini.

Aidha,amefurahishwa namna viongozi wa CBWSO ya Majengo na Mwakaganga walivyojipanga na kumaliza baadhi ya changamoto katika uendeshaji wa mradi huo ikiwamo kununua Jenereta la kusukuma maji pale umeme wa Tanesco unapokatika ili huduma ya maji kwa wananchi iweze kuendelea.

“nawapongeza sana viongozi kwa kuongeza wateja wa majumbani na vituo vya kuchotea maji,mmesaidia wananchi wengi katika vijiji hivyo viwili kupata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao”alisema Kivegalo.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa chombo cha kutoa huduma ya maji ngazi ya jamii katika kijiji cha Majengo na Mwakaganga Ester Magola alisema kabla ya kuanzishwa kwa mradi huo ,changamoto kubwa ilikuwa kupata huduma ya maji safi na salama.

Alisema,wananchi wa vijiji hivyo walilazimika kutumia maji kutoka kwenye vyanzo vya asili kama mito midogo,hata hivyo haikutosheleza mahitaji ya wananchi wa vijiji hivyo.

Katibu wa chombo cha utoaji huduma ya maji ngazi ya jamii ya kijiji cha Majengo na Mwakaganga Athuman Mtaba alieleza kuwa,vituo vyote vya kuzalisha maji vimefungiwa dira(Bulk meter)ambapo uwiano wa ufungaji wa dira hizo kwa wateja ni asilimia 100.

Alisema,huduma za maji utolewa kupitia vituo vya jamii(Dps) 16 na wastani wa mahitaji ya maji kwa wakazi wote katika eneo la huduma la CBWSO ni mita za ujazo 3,713 kwa mwezi wakati uzalishaji ni mita za ujazo 3,060 na chombo kina uwezo wa kuzalisha lita 8,960.

Alisema kuwa,hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi waishio katika eneo linalohudumiwa na CBWSO ni wastani wa asilimia 41.2 ambapo wakazi 3,010 kati ya wakazi wote 6,630 wa Majengo na Mwagakanga wanapata huduma ya maji safi na salama.
Mkurugenzi Mkuu wa Ruwasa Mhandisi Clement Kivegalo wa pili kushoto, akiangalia taarifa ya mradi wa chombo cha kutoa huduma ya maji ngazi ya jamii(CBWSO)kijiji cha Majengo na Mwakaganga wilaya ya Mbalali mkoani Mbeya wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya maji katika mikoa ya nyanda za Juu-Kusini(Ruvuma,Njombe,Iringa na Mbalali mkoani Mbeya)kushoto Mkurugenzi wa Utawala na rasilimali watu wa Ruwasa Bwai Biseko.
Katibu wa Chombo cha kutoa huduma ya maji ngazi ya jamii(CBWSO) cha Majengo na Mwakaganga wilaya ya Mbalali mkoani Mbeya Athumani Mtapa kushoto akitoa taarifa ya uendeshaji wa chombo hicho kwa Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Mhandisi Clement Kivegalo kulia,wa pili kushoto Makamu mwenyekiti wa CBWSO hiyo Ester Magola.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad