HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 12, 2022

MAAFISA WA JINSIA KUTOKA WIZARA 10 KUWA VINARA WA UPANGAJI WA BAJETI ZENYE MRENGO WA KIJINSIA

 Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umeandaa mafunzo ya siku mbili kwa maafisa wa Jinsia kutoka wizara 10 zinazohusisha jamii moja kwa moja ili kujadili namna ya uingizwaji wa Masuala ya Jinsia katika mpango wa bajeti kwenye wizara hizo kuelekea kwenye mipango ya Bajeti ya mwaka 2023/2024.

Akizungumza kwenye mafunzo hayo Afisa Programu Idara ya Mafunzo kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Anna Sangai amesema masuala ya jinsia ni masuala muhimu sana kwasababu yanahusisha makundi yote katika jamii hivo Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umeona uwakutanishe maafisa wa Jinsia kwasababu wao ndio waratibu wa masuala ya jinsia katika wizara mbalimbali kwasababu wanaelewa dhana, miongozo na mipango ambayo Serikali imeridhia ndani nan je ya nchi katika kufikia usawa wa kijinsia.

Pia amesema mafunzo hayo yatawasaidia sana maafisa wa Jinsia ile mipango itakayokuwa inapangwa hasa bajeti itakuwa inaelekeza namna ya kufikia usawa wakijinsia ambapo TGNP wamechagua Wizara mbalimbali ambazo ni Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Maji, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi nk. Kwasababu wanaamini hizo wizara zinahusiana sana namii ambayo ni watu.

“Tunapozungumzia watu katika jamii ndipo masuala ya kijinsia yanapojitokeza kwaiyo kuna changamoto mbalimbali ambazo zinahitaji kutatuliwa na Wizara husika ambapo toka mwanzo progamu , mipango na Bajeti zake zitakapokuwa zimeelekezwa kwa ajili ya kutatua hizo changamoto hivyo tunaamini hizi changamoto zitakuwa zimetatuliwa kwa kiasi kikubwa” Alisema Sangai

Naye mshiriki wa Mafunzo Afisa maendeleo ya Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dorah Meena amesema mafunzo haya niya muhimu sana na yamefanyika katika kipindi sahihi kabisa kwasababu serikali ipo karibu kabisa kwenye mchakato wa kuanza maandalizi ya kuandaa bajeti ya Mwaka wa fedha wa 2023/2024.

Amesema Wanawake ni kundo kubwa sana kweye jamii matokeo ya Sensa ya mwaka 2022 yanaonesha kuwa wanawake ni wengi kuliko Wanaume lakini bado wanakupatwa na changamoto kubwa kwenye masuala ya maendeleo yao hasa kuchangia kwenye pato la taifa.

"Tukihakikisha kwamba Bejeti za Kisekta zinazingatia usawa wa kijinsia au zinatenga fedha maalumu ili kuhakikisha masuala yakijinsia pamoja na changamoto za wanawake zinashughulikiwa katika sekta zote hasa kwenye elimu, maji, kilimo na mazingira tunaweza kuhakikisha kwamba maendeleo ya nchi na maendeleo ya kipato cha mtu mmojamoja yanakua hasa kwa mwanamke." Meena
Afisa Programu Idara ya Mafunzo kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Anna Sangai akizungumza kuhusu malengo ya mafunzo hayo kwa maafisa wa Jinsia kutoka wizara 10 pamoja na namna ya ushiriki wao kwenye vyombo vya maamuzi hasa kwenye Wizara wanazotoka kwani wao ndio wanaweza kupanga bajeti zenye mrengo wa Kijinsia wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania nakufanyika kwa siku mbili kuanzia leo tarehe 12 hadi 13 Desemba mwaka 2022 na kufanyika katika ukumbi wa ofisi za TGNP jijini Dar es Salaam.
Mtafiti wa masuala ya Bajeti na Mwanachama ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Edward Mhina akitoa mafunzo kwa maafisa wa Jinsia kutoka wizara 10 kuhusu Bejeti za Kisekta zinazingatia usawa wa kijinsia pamoja na namna ya kushiriki katika kuchochea upangaji mzuri wa bajeti yenye mrango wa Kijinsia wakati wa mafunzo ya siku mbili kuanzia leo tarehe 12 hadi 13 Desemba mwaka 2022 yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyikakatika ukumbi wa Ofisi za Mtandao huo leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakichangia mada kwenye warsha ya mafuzo kwa maafisa wa Jinsia kutoka wizara 10 yanayofanyikakwa siku mbili kuanzia tarehe 12 hadi 13 Desemba mwaka 2022 katika ukumbi wa ofisi za Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) jijini Dar es Salaam.
Afisa maendeleo ya Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dorah Meena akizungumza na waandishi wa habri kuhusu mafunzo ya siku mbili kwa maafisa wa Jinsia kutoka Wizara 10 yatakavyochochea upangaji wa Bajeti yenye mrengo wa kijinsia hasa kwa bajeti ijayo ya mwaka 2023/2024 wakati wa mafuzo yaliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) na kufanyika katika ukumbi wa Ofisi hizo leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad