DKT. MPANGO APIGILIA MSUMARI AJIRA ZA WAGENI, ATE WATOA TUZO MWAJIRI BORA 2022 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 3, 2022

DKT. MPANGO APIGILIA MSUMARI AJIRA ZA WAGENI, ATE WATOA TUZO MWAJIRI BORA 2022

 

Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango, akimkabidhi Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu wa Benki ya NMB, Emmanuel Akonaay (katikati), Tuzo ya Mwajiri Bora 2022 baada ya NMB kuibuka mshindi wa jumla katika hafla ya utoaji tuzo hizo zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na kufanyika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako. (Na Mpiga Picha Wetu).


Baadhi ya Waajiri wakifuatilia Tuzo ya Mwajiri Bora 2022  zinavyotolewa katika hafla ya utoaji tuzo hizo zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na kufanyika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya waajiri wakifurahi Tuzo ya Mwajiri Bora 2022 baada hafla ya utoaji tuzo hizo zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na kufanyika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. 

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amesema Waajiri wanapoadhimisha sherehe za mwajiri bora, wazingatia sheria zilizopo kuhusu ajira kwa wageni.

Hayo ameyasema wakati wa Hafla ya kutoa tuzo za waajiri bora kwa mwaka 2022 ziliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam leo Desemba 2, 2022. Amesema kuwa baadhi ya waajiri wamekuwa wakiajiri wageni hata katika nafasi zisizo za kitaalamu au katika kazi ambazo utaalamu unapatikana hapa nchini.

Waajiri wameaswa kuandaa kutekeleza mpango wa kuandaa wataalamu wazawa watakaochukua nafasi za wataalamu kutoka nje mara baada mikataba yao ya kazi kuisha muda wake nchini.

Pia amewahimiza waajiri wote kuboresha maslahi ya wafanyakazi kulingana na nafasi zao katika uzalishaji kwani serikali imeondoa baadhi ya tozo zilizokuwepo ili kuongeza mazingira katika uzalishaji na kuongeza tija.

Amesema ofisi ya Makamu wa Rais imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa wananchi walioachishwa kazi, waliocheleweshewa haki zao bila kufuata sheria na haki iliyocheleweshwa ni sawa na haki ilinyimwa.

“Hivyo waajiri angalieni namna mtakavyoweza kuboresha maslahi ya wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kuwapatia posho, tuzo na motisha mbalimbali kama sehemu ya kuonesha mchango wa kuwa wafanyakazi bora katika taasisi zao.”

Pia amewaasa kuzingatia sheria na kutoa mikataba ya kazi zinazostahili mkataba badala ya kuwapandisha watu kazi kama Vibarua kwa kazi ambazo wangeweza kuwa na mikataba ya kazi, aidha aiagiza wizara ya kazi kutoa elimu kwa waajiriwa kujua haki zao lakini pia kuhakiki baina ya mikataba inayotolewa katika masuala ya wajibu na haki za mwajili na haki za mwajiriwa kwenye masuala ya afya, likizo, ulemavu mafao na hata kwenye migogoro.

Pia amesisitiza suala la kuwajengea uwezo wafanyakazi na kuhakikisha wanapewa vitendea kazi vinavyohitajika ili waweze kufanya kazi vizuri na kwa usalama. Waajiri wawe na mipango mkakati wa kila mwaka kwa waajiriwa kujinoa kitaaluma ili waweze kuafanya kazi kwa ubora na ufanisi unaotegemewa na waajiri.

Amewakumbusha waajiriwa kufanya kazi kizalendo, kwa ubora na ufanisi na kujiepusha na kero za rushwa, Ufisadi, uhujumu uchumi wanchi na kufuata sharia na taratibu zilizowekwa.

Kuhusiana na vitendo vya uonevu unyanyasaji n ahata ukatili kazini amesema kuwa bado kunatabia ya uonevu na dhuruma kwa wafanyakazi, matumii mabaya ya madaraka ambayo yanasababisha wafanyakazi kuwa wanyonge katika maeneo ya kazi.

Tumeshuhudia wafanyakazi wakinyanyaswa juu ya umri, jinsia, rangi, kabila, ulemavu na dini amesema vitendo hivyo ni ukiukwaji wa haki za wafanyakazi katika utendaji wa kazi.

Katika hafla hiyo taasisi na makampuni mbalimbali wamepata tuzo za waajiri bora, Kampuni inayofuata usawa wa Kijinsi, In

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad