TVLA IMEWATAKA WAFUGAJI KUZINGATIA MATUMIZI SAHIHI YA CHANJO ZA MIFUGO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 21, 2022

TVLA IMEWATAKA WAFUGAJI KUZINGATIA MATUMIZI SAHIHI YA CHANJO ZA MIFUGO

 Meneja wa wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Kanda ya nyanda za juu kusini Dkt.Qwari Bura akiongea na waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya miaka kumi ya TVLA.


Na Fredy Mgunda,Iringa.
WAKALA wa Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) imewahimiza wafugaji kuzingatia matumizi sahihi ya chanjo za Mifugo na kuhakiki wa ubora wa vyakula ili kuepusha madhara makubwa ya kiafya yanayoweza kuwakabili walaji wa nyama hizo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa wiki ya maadhinisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa TVLA, Meneja TVLA Kanda ya nyanda za juu kusini Dkt.Qwari Bura alisema kuwa matumizi yasiyo sahihi ya chanjo na vyakula vya Mifugo yasipozingatiwa inatajwa huenda ikasababisha vifo kutokana na madhara ya nyama ambayo italiwa na binadamu.

Dr Bura alisema kuwa matumizi holela ya dawa hasa dawa za aina ya antibaiotiki huweza pia kuathiri binadamu kutokana na kula mabaki ya dawa hizo kwenye vyakula vinavyotokana na wanyama.

Alisema kuwa hilo ni tatizo kubwa linaloikabili dunia kwa sasa na wafugaji wanapaswa kuzingatia ushauri unaotolewa ili kulidhibiti. Inakadiriwa kwamba kufikia mwaka 2030, watu zaidi ya milioni 10 watakufa kila mwaka kutokana na dawa kushindwa kuwatibu kwani vimelea vya magonjwa vitakuwa vimejenga usugu unaotokana na matumizi holela ya dawa kwa binadamu na mifugo.

Dr Bura alisema kuwa wafugaji wanapaswa kuacha mara moja tabia ya kutibu wanyama wao bila vipimo ili kulinda afya ya wanyama na binadamu

Dr Bura alisema kuwa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) ni Wakala ya Serikali chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliyoanzishwa kwa Sheria ya Wakala za Serikali Na. 245 (iliyofanyiwa marekebisho Mwaka 2009) na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali la tarehe 9 Machi 2012. Wakala ilizinduliwa rasmi tarehe 11 Julai, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi ilitokana na kuunganishwa kwa iliyokuwa Maabara Kuu ya Mifugo (CVL), Vituo vya Kanda vya Uchunguzi na Utambuzi wa Magonjwa ya Mifugo (VICs), Taasisi ya Utafiti wa Ndorobo (TTRI) Tanga na Kituo cha Utafiti wa Ndorobo (TTRC) Kigoma.

alisema kuwa wakala wanavituo 11 ambavyo hutekeleza majukumu mbalimbali ya Wakala katika maeneo yao ambavyo ni Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) - KIBAHA-PWANI ambayo kazi yake pekee ni kufanya tafiti za chanjo na kuzalisha chanjo za mifugo. Maabara ya Veterinari Kanda ya Kati - DODOMA Maabara ya Veterinari Kanda ya Nyanda ya Juu Kusini – IRINGAMaabara ya Veterinari Kanda ya Ziwa - MWANZA Maabara ya Veterinari Kanda ya Kaskazini - ARUSHA Maabara ya Veterinari Kanda ya Magharibi - TABORA Maabara ya Veterinari Kanda ya Kusini – MTWARAMaabara ya kanda ya Kusini Magharibi-SUMBAWANGAMaabara ya Kanda ya Ziwa MEATU - SIMIYU. Kituo cha utafiti wa magonjwa yaenezwayo na wadudu kwenye mifugo – VVBD - KIGOMA Kituo cha utafiti wa magonjwa yaenezwayo na wadudu kwenye mifugo - VVBD- TANGA.

Dr Bura alisema kuwa watafungua Jengo Jipya la Maabara na Ofisi Kituo cha Iringa kinachohudumia Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ambayo ni mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya na Ruvuma, wafugaji wa kuku wa asili na kufanya mikutano na wafugaji kwa lengo la kutoa Elimu kuhusiana na huduma zinazotolewa na TVLA hususan huduma za upimaji wa mgaonjwa na chanjo na Kufanya upimaji wa magonjwa ya Mifugo (Bure) kwenye kituo chetu cha zamani kilichopo mtaa wa Boma Manispaa ya Iringa na Uchanjaji wa kuku (Bure) kwenye kata

Alisemakuwa wakala ikaamua kufanya maadhimisho ya miaka hiyo 10 tangu ilivyoanzishwa kwa kutenga siku tano kuanzia tarehe 21/11/2022 hadi tarehe 25/11/2022 kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwa na lengo la kuwafikia wafugaji na kurudisha kile ilichokipata kwa jamii. Maadhimisho haya yatafanyika nchi nzima kwenye vituo vyetu vya Makao Makuu na vituo 11 vya mikoani, na kila kituo kimepanga kufanya shughuli mbalimbali katika siku hizo tano kama kwa Kutoa Elimu kuhusiana na huduma zinazotolewa na TVLAKufanya upimaji wa magonjwa ya Mifugo (Bure) kwa maeneo yatakayobainishwaUchanjaji wa Mifugo (Bure) kwa maeneo yatakayobainishwaUtoaji wa Elimu ya Mifugo (Bure).

Dr Bura alimazia kwa kusema kuwa Katika kufanikisha maadhimisho haya Kituo cha Iringa kimejipanga kuwaelemisha wafugaji hususani juu ya shughuli ili kuongeza tija katika ufugaji Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, shughuli hizo ni pamoja na elimu kuhusiana na Uchunguzi na utambuzi wa Magonjwa ya Wanyama, elimu ya matumizi sahihi ya Chanjo za Mifugo, umuhimu wa uhakiki wa Ubora wa Vyakula vya Mifugo, elimu kuhusu uhakiki wa ubora, Usajili na uthibiti wa ubora wa viuatilifu vya Mifugo, na kutoa huduma za ushauri na mafunzo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad