HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 21, 2022

MWENYEJI HOIII…!!! UFUNGUZI MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA

 


Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV - Qatar
MWENYEJI wa Michuano ya Kombe la Dunia 2022, Qatar amepoteza mchezo wake wa kwanza wa ufunguzi wa Michuano hiyo baada ya kupigwa mabao 2-0 na timu ya taifa ya Ecuador kwenye mchezo wa Kundi A uliochezwa kwenye dimba la Al Bayt mjini Doha.

Qatar wameonyesha udhaifu mkubwa kwenye mchezo wao wa kwanza wa Michuano hiyo, baada ya kuruhusu mashambulizi mengi kwenye lango lao mara kwa mara, hususani kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Ecuador walianza rasmi Michuano ya Kombe la Dunia kwa kuandika bao lao la kwanza kwa mkwaju wa Penalti, kwenye dakika ya 16 baada ya Nahodha na Mshambuliaji wa timu hiyo, Enner Valencia kuangushwa na Golikipa wa Qatar, Saad Al Sheeb kwenye eneo la hatari.

Nahodha wa Ecuador, Valencia alianza kufungua ukurasa wa mabao kwa upande wake na upande wa timu yake ya taifa kwenye dakika hiyo ya 16, baada ya kuweka wavuni Penalti safiii…upande wa kulia wa lango la Qatar na kumuacha Golikipa Saad akienda upande wa kushoto.

Mshambuliaji Enner Valencia, kama mwenye bahati katika mchezo huo wa ufunguzi wa Michuano hiyo mikubwa duniani, dakika ya 31 aliandika bao la pili baada ya kupiga mpira wa Kichwa, na kuupeleka mpira huo upande wa kushoto, akiunganisha ‘Krosi’ safi iliyotoka upande wa kulia mwa lango la Qatar.

Mchezo wa pili wa mzunguko wa Kundi A, Qatar watacheza na timu ya taifa Senegal huku mzunguko wa tatu na wa mwisho watacheza na timu ya taifa ya Uholanzi.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad