GF TRUCKS & EQUIPMENTS YASAIDIA JANGA LA MOTO MLIMA KILIMANJARO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 15, 2022

GF TRUCKS & EQUIPMENTS YASAIDIA JANGA LA MOTO MLIMA KILIMANJARO

 
Na mwandishi wetu Kilimanjaro

Licha ya zoezi la uzimaji moto mlima Kilimanjaro kukamilika kwa asilimia 99 lakini vikosi mbali mbali vya jeshi la akiba pamoja na askari wa wanyamapori bado wapo eneo la tukio kuzunguka mlima kwa ajili ya doria na kuhakikisha masalia ya moto ulipo kwenye visiki wana udhibiti kwa haraka ili usilete madhara Zaidi.

Akizungumza wakati wa kupokea misaada iliyotolewa na kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd ,Kiongozi wa Geti ya Mweka Afisa mfawidhi daraja la kwanza Denis Simion aliishukurun kampuni ya GF kwa kuguswa na kupeleka misaada mbalimmbali ya vyakula kwa ajili ya askari hao wanaoendelea na zoezi la uzimaji moto

Unajua ndugu Mwandishi moto ni kama umedhibitiwa kwa asilimia 99 lakini hatuwezi viondoa vikosi vya askari wetu katika eneo la mlima kwani lolote lina weza kutokea kwa hiyo kuwa tyr kukabilianja na dharula inatakiwa askari wetu wawe doria muda wote alimaliza Denis

Nae Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano wa kampuni ya GF Smart Deus Iliguswa kutokana na ajali ya moto ya mlima Kilimanjaro hivyo wakaamua kujikusanya na kutafuta utaratiobu wa kuja kukabidhi sehemu ya mchango wao kwa wapiganaji hao ambao bado wapo eneomla tukio kwa ajili ya doria ,miongoni wa vitu ni pamoja na maji ,soda mikate sukari na vingine vingi ikiwa nisehemu ya kurudisha kwa jamii faida waliyoipata katika biashara zao

GF Ni wauzaji wa magari ya FAW ,Hong Yang na mitambo aina ya XCMG pia kamuni hiyo inaoutaratibun maalumu wa kuwakopesha magari na mitambo kwa wakandarasi wa kizalendo wenye miradi mikubwa mkononi ilikukabiliana na ushindani na makampuni makubwa ya kigeni
Meneja masoko na mawasiliano wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd , Smart Deius akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula na vifaa kwa Afisa mfawidhi daraja la kwanza na Kiongozi wa Geti ya Mweka Denis Simion wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo kwa ajili ya askari wanaoendelea na zoezi la uzimaji moto katika mlima Kilimajaro.Picha na GF


Meneja masoko na mawasiliano wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd , Smart Deius (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa askari wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo kwa ajili ya askari wanaoendelea na zoezi la uzimaji moto katika mlima Kilimajaro .Picha na GF
Meneja masoko na mawasiliano wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd , Smart Deius akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula na vifaa kwa Afisa mfawidhi daraja la kwanza na Kiongozi wa Geti ya Mweka , Denis Simion wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo kwa ajili ya askari wanaoendelea na zoezi la uzimaji moto katika mlima Kilimajaro.Picha na GF

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad