HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 3, 2022

BODI YA SHIMA YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR, WAJUMBE WAASWA KUENDELEZA SHIRIKA KIBIASHARA

 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Hamad Masauni akizungumza wakati wa kuzindua bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza (SHIMA) leo Novemba 3, 2022 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu, Said Mwema na kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchini, Dkt. Maduhu Kazi.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchini, Dkt. Maduhu Kazi akizungumza wakati wa kuzindua bodi ya shirika la Uzalishaji Mali la Magereza (SHIMA) leo Novemba 3, 2022 jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu na katibu wa Bodi ya shirika la Uzalishaji Mali la Magereza (SHIMA), Muremi Marwa akisoma historia, Mafanikio, Changamoto na Fursa za shirika la Uzalishaji Mali la Magereza (SHIMA) wakati wa Uzinduzi wa Bodi hiyo leo Novemba 3, 2022 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi wakiwa katika Uzinduzi wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza jijini Dar es Salaam leo Novemba 3, 2022.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya nchi, Hamad Masauni amewataka Wajumbe wa bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza (SHIMA) kuepuka kuwa na Shirika lisilojiendesha kibiashara.

Hayo ameyasema wakati wa Uzinduzi wa Bodi hiyo jijini Dar es Salaam leo Novemba 3, 2022. Amesema kuwa bodi hiyo inakazi pana la kusaidia Shirika kujiendesha kibiashara ili kupunguza changamoto na kutimiza malengo ya ufanisi wake wa kazi.

Amesema kuwa kazi mojawapo ya Magereza ni kurekebisha wafungwa ili wawe raia wema lakini pia waweze kuchangia katika Uzalishaji wa shirika.

Amesema kuwa jeshi la Magereza linawategemea sana bodi ya SHIMA katika kutimiza malengo yake katika utendaji na ufanisi wake wa Kazi na kuchangia Mapato Serikalini na kutengeneza ajira kwa wananchi.

"Shirika lijiendeshe kibiashara ili liweze kupunguza changamoto za Jeshi la Magereza." Amesema Masauni

Amesema kuwa anategemea bodi ya shirika hilo kufanya kazi kwa kwa karibu na Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika katika kutatua changamoto zilizopo, pia kutumia fursa zilipo ili kuliendesha kwa faida zikiwa ni pamoja na kushirikiana na sekta binafsi.

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchini, Dkt. Maduhu Kazi amesema kuwa bodi ya SHIMA kwa kushirikiana na shirika pamoja na wizara watashirikiana kwaajili ya kutatua changamoto zilipo katika Shirika.

Amesema kuwa Usimamiaji wa Rasilimali za shirika utaimalika ikiwa ni pamoja na Ufatiliaji wa sheria, taratibu, Kanuni na ili kuweza kupata Rasilimali ambazo zitatumika vizuri kwa malengo kusudiwa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu, Said Mwema amesema kuwa kutokana na uzoefu alionao watatumia changamoto zilizopo ili ziwe fursa ikiwa ni katika kutimiza malengo ya Shirika hilo.

Ameahidi kuwa watafanya kazi kwa kushirikiana na wajumbe wengine wa bodi, Wizara na Uongozi wa shirika hilo kwaajili ya kufanikisha maono na dhamira ya kuanzishwa kwa shirika la SHIMA.

"Na haya yote  yatakwenda vizuri kama Wote sisi tutafanya kazi kama ndio wenye mali, kwa kufuata Sheria, kanuni na taratibu zilizoanzisha za Kuendesha shirika la Uzalishaji uchumi la Magereza." Amesema Mwema.

Amesema kuwa Kazi ya bodi sio kuingilia kazi uongozi wa shirika bali ni chombo cha kuweka sera za kuongeza ufanisi, Uwajibikaji na utawala bora katika kutatua changamoto zilizopo katika shirika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad