HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 31, 2022

Zawadi za NMB MastaBata msimu huu kuwakwamua wateja kiuchumi

 

Msimu wa nne wa kampeni ya NMB MastaBata tayari umeanza baada ya promosheni

hiyo ya kuchagiza malipo kidijitali kuzinduliwa Mbeya Ijumaa huku sehemu ya zawadi
zenye thamani ya TZS milioni 350 ikipangwa kutumika kuwawezesha wateja kiuchumi.
Kiasi cha TZS milioni 173 na pikipiki 14 zitatumika kuwakwamua kiuchumi washindi wa
shindano hilo linalojulikana mara hii kama NMB MastaBata, Kote-Kote!
Kwa mujibu wa Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Bw Filbert Mponzi,
utaratibu huo utasaidia kuimarisha vipato vya wateja watakaoibuka washindi.
MastaBata ya mwaka huu itaua ndege wawili kwa jiwe moja. Itahamasisha matumizi
zaidi ya kadi za NMB Mastercard na Lipa Mkononi(QR) na kuwapa fursa wateja
kuboresha uchumi wao.
“Tofauti na mwaka jana, mwaka huu tumeamua kuwa na zawadi ya fedha pamoja na
pikipiki sababu tunahitaji sio tu kuhamasisha matumizi ya kadi lakini pia kuwa chachu
ya mabadiliko ya kiuchumi ya wateja wetu, tunaamini pikipiki hizi zinakwenda kutumika
katika biashara na kuongeza kipato cha washindi wetu,” Bw Mponzi alibainisha.
Zawadi kubwa itakayohitimisha kampeni ya NMB MastaBata, Kote-Kote ni washindi
saba kujishindia tiketi za kusafiri kuelekea Dubai pamoja na wenzi wao kwa siku nne
Kupitia zawadi hizo, NMB inataka na msimu unaokuja wa Krismasi na Mwaka Mpya
kufana zaidi kwa wateja wake, na kusema kwani kila wiki wateja 75 watajishindia TZS
100,000 kila mmoja, Pikipiki moja na kila mwezi 1,000,000 kila mmoja na Pikipiki 2
hivyo jumla Pikipiki 14.
Mgeni rasmi wa uzinduzi huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Dr Rashid Chuachua,
aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa, Bw Juma Homera na kuipongeza NMB kwa kuwa
mshirika wa dhati wa maendeleo kuchangia ustawi wa jamii.
Huu ni mwaka wa wanne mfululizo wa kampeni za NMB kwa kushirikiana na kampuni
ya Mastercard kuhamasisha malipo bila kutumia pesa taslimu. Mchakato huu ulianza na
MastaBata mwaka 2018, kisha MastaBata Siyo Kikawaida na kampeni ya mwaka janailikuwa ni MastaBata – KivyakoVyako.Mkuu wa wilaya ya Mbeya Dr. Rashid Chuachua (wapili kulia) akifurahia baada ya kuzindua rasmi kampeni ya NMB Mastabta – Kotekote iliyozinduliwa kitaifa mkoani Mbeya yenye lengo la kuhamasisha malipo ya bidhaa na huduma kwa kutumia kadi, kuskani QR (Lipa Mkononi) na malipo ya kimtandao. Benki ya NMB Imetenga zawadi za zaidi ya milioni 300 kwaajili ya kampeni hii. Wapili kushoto ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa benki ya NMB, Filbert Mponzi, kulia ni Afisa Mkuu wa Rasilimali watu wa benki hiyo, Emmanuel Akonaay na kushoto ni Mkuu wa Idara ya Kadi, Philbert Casmir.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad