WAZIRI BALOZI PINDI CHANA AKUTANA NA KAMATI YA KITAIFA YA MAANDALIZI YA ONESHO LA UTALII LA KIMATAIFA LA SITE - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 16, 2022

WAZIRI BALOZI PINDI CHANA AKUTANA NA KAMATI YA KITAIFA YA MAANDALIZI YA ONESHO LA UTALII LA KIMATAIFA LA SITE

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.  Balozi Dkt. Pindi Chana amekutana na Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Onesho la utalii la Kimataifa linalojulika kama “Swahili International Tourism Expo (SITE)” kwa lengo la kupata taarifa ya maandilizi yanayofanywa na kamati hiyo. Onesho hilo la Utalii linatarajia kufanyika katika Ukumbi  wa Mikutano wa Mlimani City uliopo jijini Dar Es Salaam  tarehe 21 hadi  23 Oktoba,  2022. 

Akizungumza na Wajumbe wa Kamati hiyo, Balozi Dkt. Pindi Chana amewasisitizia wajitume  na kuhakikisha onesho hilo linafanyika kwa kiwango cha kimataifa.

 “Nategemea kuona taasisi zote za Wizara ya Maliasili zinahamasisha  wadau wao kushiriki katika onesho hili na kutumia fursa hii kufanya biashara na wadau wa utalii  kutoka nchi mbalimbali duniani waliothibitisha kushiriki  katika onesho la mwaka huu”.


Amesema Serikali imedhamiria  kuwanyanyua wafanyabiashara za utali wa Tanzania kwa kuendelea kuandaa onesho la sita ambalo linaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassani za kuanzisha programu ya The Royal Tour Tanzania inayotangaza utalii wa Tanzania.  


Ameongeza kuwa Kamati hiyo imepewa dhamana na kuaminiwa, hivyo lazima kila mjumbe apambane na kuhakikisha anatekeleza jukumu alilopangiwa. Amebainisha kuwa kamati hiyo imeshirikisha taasisi zote muhimu ambazo zina mchango mkubwa wa kufanikisha Site 2022. 


Onesho la kwanza la Swahili International Tourism Expo lilifanyika mwaka 2014  katika Ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es salaam


Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.  Balozi Dkt. Pindi Chana ameongozana na Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utlalii Tanzania pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania, Felix John (Kulia)  Idara ya Utalii (kushoto) Rich Wandwi na kakikagua eneo litakalotumika kwaajili ya SITE 2022. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.  Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea na wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Maandaizi ya Onesho la SITE katika ukumbi wa Milimani City jijini Dar es Salaam

Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya kitaifa wakifuatilia maagizo ya anayootolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.  Balozi Dkt. Pindi ChanaWaziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.  Balozi Dkt. Pindi Chana akikagua mbalimbalikatika

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad