HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 30, 2022

WAHITIMU 84 WA CHUO CHA UHANDISI NA TEKNOLOJIA AL-MAKTOUM WATUNUKIWA VYETI, WASHAURIWA WASIBWETEKE

 

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WAHITIMU 84 wa fani mbalimbali katika Chuo cha Uhandisi na Teknolojia cha Al Maktoum(AMCET)wametunukiwa vyeti vya taaluma baada kuhitimu na kukidhi vigezo vyote vilivyoanishwa kwa mujibu wa NACTVET.

Akizungumza kwenye mahafali ya Tisa ya Chuo hicho Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Kheri Mahimbali kwa niaba ya Waziri wa Nishati Januari Makamba aliyekuwa mgeni rasmi, amewakumbusha wahitimu baada ya kuondoka chuoni hapo wasibwete bali watumie fursa zilizopo ikiwemo kujiajiri na kujiendeleza kwenye masomo..

Hivyo amewaomba wahitimu wazingatie matumizi bora ya elimu na ujuzi walioupata kwenye chuo hicho na wawe kujifunza huko waendako kwani elimu haina mwisho na teknolojia zinabadilika kila uchwao.

“Jumla ya wahitimu 84 leo wametunukiwa vyeti vya ngazi ya Astashahada na Stashahada katika fani mbalimbali nakupongezi sana , na nimefamishwa kuwa karibu nusu ya wahitimu waliotunukiwa vyeti vyao ni watumishi wa Wizara ya Nishati, nakupongezeni, natumai mtaongeza ufanisi katika kazi zenu na kufanya kazi kwa weledi kwa maslahi ya nchi yetu,”amesema.

Aidha amewahimiza wanafunzi wanaoendelea na masomo kuendelea kujituma katika masomo yao na hivyo kuchangia chuo hicho kufikia malengo yake na kufanikisha kufikiwa kwa malengo yao na Taifa kwa ujumla.

Amesema kuwa amesikia changamoto za chuo hicho ambazo ni kupata udahili mdogo wa wanafunzi, kutokuwepo kwa mikopo kwa wanafunzi wa Stashahada , uhaba na upatikanaji wa sehemu za kujifunzia kwa vitendo viwandani kwa ajili ya wanafunzi na wakufunzi pamoja na chuo kushindwa kupata bunifu zinazolenga kutatua matatizo ya teknolojia yanayokabili taasisi mbalimbali nchini.

“Napenda kuwaambia kuwa tutaangalia namna ya kukisaidia chuo hiki ili kiweze kubadili changamoto hizo kwani hiki ni chuo chetu Kuhusu changamoto za chuo hicho, amesema Mahimbali na kuipongeza jamii ya Chuo cha Al-Maktoum chini ya uongozi wa Dk.Hamdun Sulayman kwa kukiweka chuo hicho katika mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia.

Awali Mkuu wa Chuo hicho Dk.Sulayman amesema mwaka wa masomo 2010/2011 chuo kilianza kutoa wanafunzi katika fani ya teknolojia ya habari na miaka iliyofuata kuongeza kutoa mafunzo katika fani za uhandisi umeme, eletroniki na mawasiliano , mfumo wa habari na teknolojia ya mawasiliano na sayansi ya maabara , teknolojia katika ngazi ya Astahahada na Stashahada.

Ameongeza Chuo pia kinatoa mafunzo katika ngazi ya ufundi stadi kwenye fani za umeme. Eletroniki na teknolojia ya habari na mawasiliano katika kipindi cha mwaka wa masomo 2010/20211 hadi 2020/2021 jumla ya wanafunzi 545 walihitimu masomo yao na kati yao wasichana 58 na wavulana 487.“Na leo hii wanahitimu wanafunzi 84 wa mwaka masomo 2021/2022 kati yao wakiwemo wasichana 13 na wavulana 71.”

Aidha amesema katika kukabiliana na changamoto zilizopo amesema chuo kinafanya kampeni mashuleni kuhamasisha wanafunzi kupenda masomo ya sayansi lakini pia kuhamasisha wahitimu wa ufundi stadi kujiunga AMCET kuendeleza masomo yao katika ngazi ya Stashahada , pia chuo kinafanya ushirikiano na kampuni mbalimbali ili ziweze kuwapatia wanafunzi wao kujifunza masomo kwa vitendo viwandani.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho Profesa Hamis Dihenga amesema dira yao ni kuwa chuo kinachoongoza kwenye utoaji wa elimu ya ufundi katika Afrika Mashariki .Dhima ya chuo ni kutoa elimu ya ufundi yenye kuambatana na maadili mema.

“Ili kufikia matarajio tuliyojiwekea chuo chetu kinampanga mkakati unaolenga yafuatayo; kutoa taaluma ,ushauri na utafiti , kuwa na miundombinu bora ya kufundisha na kujifunzia, kujenga ushirikiano na wadau pamoja na kukitambulisha chuo kiweze kujulikana,”

Pia amesema Chuo chuo kinaamini kuwa mafunzo ya uhandisi na teknolojia ni lazima yaambatane na misingi ya maadili ambayo wamejiwekea ikiwemo kujenga utashi wa kufanya kazi kwa pamoja, uwajibikaji , kusimamia ubora wa kazi, kuchagiza umuhimu wa kutumia busara na hekima katika utendaji na kuhimiza ubunifu.Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Kheri Mahimbali akizungumza kwenye mahafali hayo ya Tisa ya Chuo cha Uhandisi na Teknolojia cha Al-Maktoum (AMCET) yaliyofanyika kwenye chuo hicho kilichopo Mbezi Tangibovu.Mahimbali amemwakilisha Waziri wa Nishati Januari Makamba ambaye alikuwa mgeni rasmi.Katika mahafali hayo wahitimu 84 wametunikia vyeti vyao vya kitaaluma.Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Kheri Mahimbali akimtunuku cheti mmoja ya wahitimu waliomaliza masomo kwenye chuo cha  Uhandisi na Teknolojia cha Al-Maktoum (AMCET) yaliyofanyika kwenye chuo hicho kilichopo Mbezi Tangibovu. Mahimbali amemwakilisha Waziri wa Nishati Januari Makamba aliyekuwa mgeni rasmi.: Mkuu wa Chuo cha  Al-Maktoum Dk.Hamdun Sulayman akizungumza kabla ya wahitimu kutunukiwa vyeti vyao vya kitaaluma baada ya kuhitimu kwenye chuo hicho. Baadhi ya wahtimu wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea wakati wa mahafali ya tisa ya Chuo cha Al-Maktoum kilichopo Mbezi Tangibovu mkoani Dar es Salaam .Jumla ya wahitimu 84 wa fani mbalimbali wametunukiwa vyeti vyao vya kitaaluma.Wanafunzi wa Chuo cha Uhandisi na Teknolojia  cha Al-Maktoum wakiimba shairi maalumu ambalo limeaandaliwa kwa ajili ya kusherehesha mahafali ya Tisa ya Chuo hicho yaliyofanyika leo.Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho Profesa.Hamis Dihenga(kushoto) akitafakari jambo wakati wa mahafali hayo .Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Kheri Mahimbali(wa nne kushoto) akiwa amesimama pamoja na viongozi wengine wa Chuo hicho wakati wahitimu wa fani mbalimbali wakitunukiwa vyeti vyao vya kitaaluma baada ya kuhitimi masomo yao.Viongozi wa Chuo cha Al-Maktoun wakiwa  na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Kheri Mahimbali pamoja na watumishi wa Chuo hicho waliosimama baada ya kumalizika kwa Mahafali ya Tisa ya chuo hicho.




Wanafunzi wa Kituo cha Ubunifu katika Chuo hicho wakionesha ubunifu wao kwa mgeni rasmi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Kheri Mahimbali(aliyevaa miwani) wakati wa mahafali ya tisa ya chuo cha Uhandisi na Teknolojia cha Al-Maktoum(PICHA ZOTE NA SAID MWISHEHE) 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad