HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 4, 2022

WAFANYAKAZI UDSM NDAKI YA SAYANSI ZA JAMII WAWATEMBELEA WARAIBU WA DAWA ZA KULEVYA KIGAMBONI

Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Christine Noe Pallangyo akizungmza leo Oktoba 4, 2022 kabla ya kukabidhi msaada wa kibinadamu ikiwa ni kuadhimisha miaka 60 ya chuo kikuu cha Dar es Salaam na kuadhimisha miaka 57 tangu kuanzishwa kwa Ndaki ya Sayansi za Jamii.Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
KATIKA kuadhimisha miaka 60 ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, wahadhiri na wafanyakazi na Wanachuo wa Ndaki ya Sayansi za Jamii watembelea Kituo cha Vijana walioathirika na Uraibu wa dawa za Kulevya cha Muungano Recovery Community (MCR) kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Katika safari ya kutembelea kituo hicho leo Oktoba 4, 2022 wafanyakazi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii wametoa elimu juu ya masuala ya afya ya akili na matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana waliokutwa katika kituo cha MCR.

Akizungumza na waandishi wa habari Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Christine Noe Pallangyo amesema kuwa kufika katika kituo hicho ni kuonesha ushirikiano na walezi pamoja na waraibu wa dawa za kulevya ikiwa ni maadhimisho ya miaka 60 ya chuo hicho pamoja na Ndaki ya Sayansi za Jamii ambayo inatimiza Miaka 57 tangu kuanzishwa kwake.

"Sisi tunahusika moja kwa moja na tafiti zinazohusiana na jamii zetu na matatizo yaliyopo kwenye jamii.Amesema Profesa Pallangyo, amesema hiyo ni sehemu ya kuelewa matatizo ya jamii na kujifunza kwa undani na kushirikiana na jamii ambazo wanazifanyia utafiti kila wakati pamoja na kujiunganisha na jamii wanazozihudumia.

Katika ziara hiyo ya kuwatembelea waraibu wa dawa za kulevya wametoa msaada wa vitu mbalimbali ya chakula, Usafi pamoja na msaada wa elimu ya Kisaikolojia na afya ya Akili.

"Tukio hili la leo linaonesha utayari wa kushirikiana kuijali jamii, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hasa ndaki ya Sayansi za Jamii ina jali jamii ambayo tunafanyanao kazi." Ameeleza

Akizungumzia nafasi ya Ndaki hiyo katika jamii amesema kuwa wanatoa mafunzo na wanawataalamu ambao wanafanya kazi na jamii na kila mwaka wataalamu wa Sosiolojia wanahitimu katika chuo hicho ambao pia wanafanya kazi na jamii.

Amesem Kuwa wanawataalamu wa kitafiti pamoja na Kamati katika chuo inayotoa elimu ya Saikolojia na wataalamu wa kutoa huduma na wataalamu ambao wamesoma UDSM.

Kwa Upande wa Meneja wa Kituo cha Muungano Recovery Community, Kigamboni, Khamis Agib amewashushukuru Wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ndaki ya Sayansi za Jamii kwa kuwapelekea Msaada huo.

"Kwetu sisi tunaona kitu kikubwa sana walichotufanyia ingawa wao wanaona ni kidogo. tunashukuru kwa kutuchagua sisi kwani kunavituo vingi ambavyo wangeweza kupeleka wameonesha upendo kwa vijana ambao wanauraibu wa dawa za kulevya." Amesema Agib licha ya shukrani Agib ameiomba jamii kuacha matumizi ya vileo na dawa za kulevya kwani zinamaliza nguvu kazi ya jamii na taifa kwa ujumla pamoja ka kudhoofisha afya ya mwili na akili.

Kwa Upande wa Mratibu wa Afya ya Akili Kigamboni na Daktari wa Hospitali ya Vijibweni, Dkt. Fransis Mwita amesema kuwa waraibu wa Dawa za kulevya na vilevi na wenye matatizo ya afya ya akili wanaweza kutibiwa na wakapona kabisa hivyo ameiomba jamii kuwapeleka katika vituuo vya afya ili waweze kupata huduma hiyo.

Kwa Upande wa Mhadhiri Msaidizi wa ndaki ya Sayansi za Jamii na Rais wa Chama cha wanasaikolojia Tanzania, Mandolanga Shegembe amesema vijana wanajiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya na vileo kwa kukosa Elimu hivyo amewaomba wataalamuu waweze kutoa elimu juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya kabla vijana hawajaingia katika dimbwi hilo.

Pia ameisa jamii kuwapeleka watu wenye matatizo ya afya ya akili na waraibu wa dawa za kulevya katika vituo vya afya kwani wanaweza kutibia na wakapona kabisa.

Waliokuwa waraibu wa dawa za Kulevya Najima Libenega na Musa Kambaya wamesema kuwa jamii itambue na kumuamini kuwa ameacha dawa za kulevya.

Pia ameiomba serikali na jamii kuwaamini pale wanapoomba kazi waweze kuwaajili ili waweze kujipatia kipato kitakacho wawezesha kumudu maisha.
Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Christine Noe Pallangyo akiwakabidhi wawakilishi wa waraibu wa Dawa za Kulevya waliopo katika Kituo cha Muungano Recovery Community (MCR) kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi chuo Kikuu ch Dar eS Salaam wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutemblea kituo cha waraibu wa dawa za kulevya cha Muungano Recovery Community (MCR) leo Oktoba 4, 2022.
Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Christine Noe Pallangyo akizungumza leo Oktoba 4, 2022 kutemblea kituo cha waraibu wa dawa za kulevya cha Muungano Recovery Community (MCR).
Mratibu wa Afya ya Akili Kigamboni na Daktari wa Hospitali ya Vijibweni, Dkt. Fransis Mwita akizungmza mara baada ya kutemblea kituo cha waraibu wa dawa za kulevya cha Muungano Recovery Community (MCR) leo Oktoba 4, 2022.
Mraibu wa dawa za Kulevya Musa Kambaya aliyepo katika kituo cha Waraibu wa Dawa za kulevya cha Muungano Recovery Community chaa kigamboni jijini Dar es Salaam akizungumza mara baada ya kutembelewa na Wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Ndaki ya Sayansi za jamii.
Mraibu wa dawa za Kulevya Najima Libenega aliyepo katika kituo cha Waraibu wa Dawa za kulevya cha Muungano Recovery Community chaa kigamboni jijini Dar es Salaam akizungumza mara baada ya kutembelewa na Wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Ndaki ya Sayansi za jamii.
Mhadhiri Msaidizi wa ndaki ya Sayansi za Jamii na Rais wa Chama cha wanasaikolojia Tanzania, Mandolanga Shegembe akitoa elimu ya afya ya akili kwa waraibu wa dawa za kulevya leo walipowatembelea katika kituo cha Muungano Recovery Community (MRC)

Baadhi ya waliokuwa waraibu wa Dawa za kulevya wakiwasikiliza wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Ndaki ya Sayansi za jamii leo Oktoba 4, 2022.




Baadhi ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Ndaki ya Sayansi za jamii leo walipotembelea kituo cha Muungano Recovery Community (MRC).
Mhadhiri wa Idara ya Sosiolojia, Ndaki ya Sayansi za Jamii, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Egidius Kamanyi akizungmza walipotembelea kituo cha waraibu wa dawa za kulevya cha Muungano Recovery Community (MRC) leo Oktoba 4, 2022 Kigamboni jijini Dar es Salaam.



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad